Mhusika Kidawa na sifa zake katika hadithi Masharti ya Kisasa-Alifa Chokocho
Answer Text: Mhusika Kidawa katika hadithi “Masharti ya Kisasa”-Alifa ChokochoMwanamke mrembo ambaye alitaka kuolewa na wanaume wengi. Aliwakataa na kuwachuja hadi akamchagua Dadi. Yeye alisoma hadi kidato cha nne.Sifa za KidawaNi mzingatifu: anajua alitaka nini maishani na akazingatia matakwa yake ya ndoa ya kisasa.Alithamini ndoa yake: ili kuiauni ndoa yake anaamua kwenda kujiuzulu kazi ya umetroni pale kazini.Ni mwenye bidii: Anaifanya kazi ya ziada pale mtaani wakati hayupo kazini ili kuikimu familia yake na Dadi.Ni jasiri: mwacha mila ni jasiri. Hakuyumbishwa na umbeya wa wanajamii kama Dadi bali aliendelea kuishughulikia familia yake.