Sifa za mhusika Dadi katika hadithi Masharti ya Kisasa-Alifa Chokocho
Answer Text: Sifa za mhusika Dadi katika hadithi “Masharti ya Kisasa”-Alifa Chokocho-Huyu ni mchuuza samaki. Alimpenda mwanamke mmoja Kidawa kupita kiasi. Dadi alijaribu kumpata Kidawa kwa kila njia lakini hakuweza.-Ana bidii maishani:anachuuza samaki kwa bidii hadi wamalizike ilikumsaidia ayakimu maisha ya aila yake Kidawa.-Mwenye msimamo hasi: anayumbishwa na maneno ya watu hadi akakosa raba kabisa.-Ni jasiri: anaamua kumfuata mkewe Kidawa hadi chuoni ili kupata ukweli wa mambo.-Ni mdadisi: Anachunguza hali ya mkewe na sababu ya kujirembesha akitoka kuelekea kazini.