Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Masharti ya Kisasa (Alifa Chokocho)

Muhtasari wa hadithi, Masharti ya kisasa-Alifa Chokocho

 (12m 45s)
2984 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
MASHARTI YA KISASA-Alifa Chokocho
Muhtasari
-Kisa hiki kinahusu Kidawa mwanamke mrembo ambaye alipendwa na mvuvi na muuza samaki aitwaye Dadi.
-Dadi alimpenda sana Kidawa na akataka amchumbie awe mkewe. Kidawa alimkataa
Dadi na kumkwepa kabisa. Hata hivyo mambo yalibadilika ambayo
yalimshangaza sana Dadi.
-Kidawa alimwambia kwamba yu radhi kuolewa na Dadi kwa masharti ya ndoa ya kisasa. Dadi kwa shangwe alizonazo hakuzingatia undani wa Kidawa " Ujue kwamba mimi ni mwanamke wa kisasa, na mwanamke wa kisasa hutafuta mwanamume wa kisasa mwenye mapenzi ya kisasa.
Dadi akamwoa Kidawa mwanamke wa kisasa. Baadhi
ya mambo aliyotakiwa kuyatekeleza ni kusaidia kazi za nyumbani, kukuna nazi, kuosha vyombo, kufua na kupiga pasi. Pia amruhusu Kidawa afanye kazi ya umetroni kwa Shule ya wasichana usiku. Kidawa alifanya kazi hio kwa zamu.
- Aidha kidawa akawa na biashara ya kutembeza bidhaa za Uarabuni mitaani. Kidawa aliyafanya haya ili
"Kuunganisha ncha nyingi za mahltaji ya maisha " Baada ya miaka tisa ya ndoa, Dadi alianza kuingiwa na shaka. Akamshuku
Kidawa, akachukia kujipamba kwake, akachukia kwenda kufanya kazi usiku, akachukia alivyosimama na kuongea na wanaume wengine na vile vile akachukia uchuuzi wa bidhaa alizofanya.
Furaha ile ya kumwoa Kidawa hadi akaitwa Dadi
kichekacheka kwa kumpata mke wa kisasa Kidawa ikamtoka. Chakula kikamshinda jioni moja. Masharti ya kuosha vyombo kwa zamu pia yakamshinda.
Dadi alimfuata Kidawa kazini ili kumfumania na mwalimu mkuu kama alivyoshuku.
- Dadi akaenda nyumbani kwa mwalimu mkuu akaelezwa hakuweko. Ana kazi zilizomzidi shuleni. Dadi akawa na hakika ya kuwa mtego wake ungenasa. Mpango wake wa awali alivyopanga — akapanda paipu inayoelekea gorofani ili amwone mwalimu mkuu na Kidawa wake. Dadi alikosea
mwalimu alikuWa peke yake na rundo Ia karatasi akisahihisha.
-Kidawa alipojitoma ndani alitaka kujiuzulu kazi kwa kuwa mumewe anamshuku.
Dadi alionekana juu ya paipu "Wewe nani? Unachungulia nini hapo juu? Wewe mwizi, nini? Au mpiga bodi... Nyinyi walinzi bwenini kuna mtu amepanda juu ya paipai anachungulia ndani"
Sauti iliwavutia Kidawa na mwalimu mkuu.
- Kidawa akakuta ni mumewe. Dadi aliangukia kokoto na damu ikamtoka kichwani.
Mwalimu mkuu akapiga simu kuita ambulensi.


|