Wahusika na sifa zao katika hadithi fupi ya Shogake Dada ana Ndevu
Answer Text: Wahusika na sifa zao katika hadithi fupi ya “Shogake Dada ana Ndevu”Safia-Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.-Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote-Katika masomo yake alikuwa anaongoza darasa.Sifa za Safia-Ni mwenye tamaa: anatamani kufanya mapenzi na akatumia hila kutimiza lengo lake. Alikuwa amejivika ngozi ya kondoo nje, ndani mbwa mwitu.-Ni mjanja: anatumia maarifa na hila za kila namna ili kupata fursa ya kufanya mapenzi.-Ni mwenye hasira: Bi. Hamida anapomdadisi kuhusu hali yake ya kutapika, anapandisha hasira na kukimbia chumbani mwake.-Ni mwongo: anadanganya kuwa ana malaria suguAnadanganya kuwa Kimwana anakuja ili wajadiliane kumbe anayekuja ni mvulana mwenye ndevu na wanafanya mapenzi.-Ni muuaji: anatoa mimba na kukidhulumu kiumbe kisicho na hatia. Mambo hayakwenda sawa na yeye akafariki.-Ana ubinafsi: anafikiria yeye tu bila kujua madhara ya kiumbe kilichomo ndani tumboni mwake.Umuhimu wa Safia katika hadithi “Shogake Dada ana Ndevu”-Alifa ChokochoAnatuonya kuwa ujanja na hila zina mwisho wake. Mara nyingi huwa na mwisho mbaya.-Anawapofua vijana kuona uovu wa kuavya mimba.-Anatumika kuonya vijana kuhusu udanganyifu.-Anawasilisha ubaya wa unafiki miongoni mwa vijana.