Ufaafu wa anwani Shogake Dada ana Ndevu
Answer Text: Ufaafu wa anwani “Shogake Dada ana Ndevu”-Alifa Chokocho-Anwani ya hadithi hii inasadifu yale yaliyomo. Safia binti wa Bwana Masudi na Bi.- Hamida anajulikana kuwa ana nidhamu ya hali ya juu. Ni mtiifu, anafanya kazi zote za nyumbani na shuleni anaongoza. Wazazi hawa walijua fika kuwa Mungu amewajalia. Kwa imani yadini, Safia alikuwa mcha Mungu kabisa.-Ili kujitayarisha na mtihani wake wa mwisho, Safia aliomba rafiki yake aje kwao wadurusu pamoja.- Wazazi wake bila shaka wakamkubalia. Kimwana aliyeaminika kuwa na tabia kama ya Safia akawa anakuja kudurusu. Wakimaliza alirejea kwao. Kuzuia usumbufu wa Lulua ndugu mdogo wa Safia, wazazi wakawaruhusu kujifungia ndani.-Safia alianza kuwa mnyonge na kutapika. Alipomshirikisha mumewe, naye Lulua wakati walicheza aliwahi kujitoma chumbani akawakuta Safia na shogake wamelala na shogake ana ndevu.Safia alikuwa mjamzito na katika shughuli za kutoa akafariki. Mimba ni ya shogake mwenye ndevu.