Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Shogake dada ana ndevu (Alifa Chokocho)

Maudhui makuu katika hadithi ya Shogake dada ana ndevu

 (14m 30s)
12674 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Maudhui makuu katika hadithi ya “Shogake Dada ana Ndevu”-Alifa Chokocho
(a) Unafiki na Uongo
-Safia alikuwa mnafiki na mwongo. Alijifanya kwamba ana tabia safi kama umande, kumbe alikuwa na tamaa ya ngono Wanakijiji wanamsema vibaya mtoto wa Hamida Chechei na kumfananisha na mbwa. Hawakumsengenya Safia kwa sababu mbele ya macho yao alikuwa na tabia
nzuri. Mama anapomuuliza na kumdhihirishia kwamba anamshuku, anapandisha hasira.
(b) Tamaa za vijana
-Safia anajitahidi kwa kila jambo, masomo aliyamudu vyema. Anasifika kwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kufua, kupiga pasi na kadhalika. Kanuni au sheria za dini alizizingatia bila
wahaka (wasiwasi) wowote. Hata hivyo anawaka tamaa ya kufanya mapenzi. Anaamua kutumia ujanja kwa kutoa ombi ambalo halikuwa na shaka kwa wazazi wake. Na yeye akajichimbia kaburi mwenyewe
(c) Umbea baina ya wanajamii
-Bi. Hamida na wanawake wengine wa mtaani walikuwa
wambea. Wamemkashifu na kumuumbua Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei. Wanamwita kwamba yeye ni mbwa koko na uovu wake umezidi wa shetani. Bi. Hamida baada ya mtoto wake Safia kumwendea kinyume hataweza kusema lolote.
(d) Bidii katika Kazi
-Kutia bidii katika shughuli yoyote zile huleta tija. Awali
bidii masomo zilimpatia sifa nzuri Safia kwa sababu alikuwa wa kwanza hadi mwaka wa mwisho. Aidha bidii yake ya kazi za nyumbani,staha yake na ucha Mungu ulitambuliwa na kila mtu.
(e)Mikasa Maishani
-Bw. Masudi na Bi. Hamida walikuwa na maisha ya utulivu.Wanandoa hawa
wawili walikuwa wanaelewana. Upendo na ushirikiano wao hujidhihirisha kwa vile wanavyozungumzia mambo mazito ya nafsi zao. Baada ya kufurahia mwenendo wa binti yao — furaha inakatika ghafla.
(f) Uozo baina ya vijana
-Vijana mara nyingi huwa na mihemko ya kupapia mambo kabla ya wakati. Mkadi
alikuwa na mwenendo usiofaa.Wanawake wambea akiwemo Bi. Hamida wakamsengenya.Safia naye katafuta njia ya kukidhi tamaa zake kwa njia mwafaka. Wazazi wake mwenyewe wakarahisisha mambo kwa kuwapa ruhusa ya kujifungia ndani. Sio rahisi kutambua mienendo ya vijana. Ni vyema kuviepuka vitendo viovu maana matokeo ya uovu hayafichiki.


|