Muhtasari wa hadithi shogake dada ana ndevu
Answer Text: SHOGAKE DADA ANA NDEVU —Alifa ChokochoMuhtasari-Bwana Masudi na Bi. Hamida ni mtu na mkewe. Wamejaliwa kupata binti aitwaye Safia.- Kabla ya kulala wazazi hawa huzungumzia mambo mazito yanayogusa mioyo yao. -Walimsifia sana binti yao kwa vile alivyo na mwenendo mzuri.- Safia ana tabia inayowafurahisha wazazi wake. Shuleni anafanya vyema kabisa. Wazazi hawa walielewa vyema kabisa kuwa kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti ".Walijadili ukweli kwamba wapo wazazi waliojali wa watoto, lakini wakawa balaa. Wakakosa manufaa kwa wazee wao na jamii nzima.Bi. Hamida anatoa mfano wa mtoto wa Habiba Chechei aitwayeMkadi. Mkadi ana vitendo viovu kushinda shetani. Walimlinganisha-Mkadi na Safia na kuona binti yao ni safi hana doa.Sifa nzuri za Safia zilienea hadi kwa marafiki na watu wote wanaoingia na kutoka kwa Bwana na Bi. Masudi.Hayo yote aliyalifanya wazazi wake wakashukuru kupita kiasi.-Safia aliwataka wazazi wake wamruhusu Kimwana shoga yake aje ili wajitayarishe vyema kwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza.-Wazazi wa Safia walikubali wasemavyo wahenga kuwa, . kidole kimoja hakivunji chawa. Analolijua Safia, Kimwana halijui.analolitambua Kimwana Safia hana habari nalo.-Kimwana akaanza kuja nyumbani kwa akina Safia na wakawa wanasomea chumbani. Wakaomba kufunga mlango ili wasisumbuliwe na Lulua, ndugu mdogo wa Safia. Wazazi wao wakawaruhusu wafunge mlango kwa ndani. -Baada ya muda kupita, Bi. Hamida akawa ana shaka yakuwa Safia ni mjamzito. Akaanza kuona dalili zote kutapika na kunyong'onyea na hana uchangamfu.- Alipomdadisi, Safia alikasirika na kumlaumu mama yake. Hata hivyo Bi.- Hamida alitia shaka, akachanganyikiwa-Safia anasema uongo au ukweli. Alimuuliza mumewe, ambaye alisema kuwa Safia hawezi kuwa mjamzito. Siku moja wakila chamcha, Lulua alitoboa siri kwamba, aliingia chumbani mwa Safia akawakuta wamelala. -Na shogake Safia alimwona ana ndevu. Wakati huo huo Bw. Masudi akapata ujumbe kwa simu uliomgutusha Safia aliyekwenda kliniki kutoa mimba amekufa. Bi. Hamida na Bw. Masudi wakachukue maiti.