Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya Tumbo Lisiloshiba
Answer Text: Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya “Tumbo Lisiloshiba”Taharuki:-Hadithi inapoanza kuna taharuki. Huo ni uvumi gani? Unazushwa na nani kwa sababu gani? Anaposema haukuwa wa kupasuka bomu au kulipuka mzinga anaendelea kuitilia uzito taharuki hiyo.-Taharuki nyingine ni ile ya jitu liloingia mkahawa mshenzi lilitokea wapi.Kwa nini liliamua kuutembelea siku hiyo. Je ziara yake ni kula tu chakula au kufanya uchunguzi.Taswira:Ni mbinu ya kujenga picha akilini mwa wasomaji.-Kuna taswira nyingi katika kisa hiki. Kuna taswira ya jitula miraba mine kutokana na maelezo ya lile jitu lilivaa suti nyeusi na shati jeupe. Wakati mabuldoza yalipokuwa yakiangusha vibanda na kuwatimua watu. Ni taswira inayoangazia jinsi haki za wanyonge zinavyofifishwa. Aidha jeshi la polisi hushadidia jambo hilo hilo la unyanyasaji wa wanyonge.Balagha-Haya ni maswali yasiyohitaji majibu moja kwa moja.-Mifano: yote hayo lakini yafae nini mbele ya nia ya kuhakikisha nafasi za biashara na malengo ya starehe ya wakubwa-Chupa mbili za Coca Cola zifae nini kwa jitu kuza kama hiloMdokezo:-Maelezo machache ambayo hayakamiliki, yakitumiwa kuashiria jambo fulani. Lile jitu la miraba minne lilidokeza kwamba kungekuwa na tukio fulani. Kesho kama sote tutaamka salama.Tashbihi:-Bweu lilipasuka kama mzinga-Kiti kilionekana kama cha Shule ya chekecheaKuchanganya ndimi:Mbinu ya kuitumia lugha Zaidi ya moja katika kifungu.-Chauffeur-AudiQ7-Coca Cola-Departmental stores, casinosMethali –Ni mbinu ya lugha ambapo maneno huwa yamebeba ujumbe wa kina kando na ule unaojitokeza kwa juu juu.Kuna matumizi ya methali kama kimya kingi kina mshindoTakriri –Huu ni urudiaji kwa madhumuni ya kusisitiza-“Hawawezi, hawawezi kabisa hawawezi”Mbinu rejeshi:-Uvumi kuhusu kubomolewa kwa vibanda ulianza halafuukatoweka. Baadaye uvumi huo unarejelewa tena katika kibanda cha Mzee Mago.Chuku:-Ni mbinu ya kutia chumvi katika maneno.-Ukubwa wa tumbo la mtu mwenye miraba mine limetiliwa.Chuku:Kwa nini mwandishi amefanya hivi? jinsililivyolamba sahani zote — halikubakisha hata ishara ya chembe moja ya chakula chochote alichokula.