Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Tumbo Lisiloshiba (Said A. Mohammed)

Maudhui katika hadithi fupi ya Tumbo Lisiloshiba

 (8m 7s)
14988 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Maudhui katika hadithi fupi ya “Tumbo Lisiloshiba”
-Wakazi wa Madongoporomoka wanadhulumiwa ardhi yao. Tabaka la mabwenyenye wanawatoa katika ardhi yao na kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
Matabaka:
- Hadithi hii inasawiri kuwepo kwa matabaka katika jamii. Kuna tabaka la mabwenyeye
na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi hii jitu kubwa linaonekana likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka.
Ukosefu wa Haki:
-Katika jamii iliyojaa dhuluma hakuna haki. Watu wa Madongoporomoka wanaporwa haki yao ya kumiliki ardhi.
Ardhi inatwaliwa na wenye nacho. Hata wanaposhauriana kutafuta wanasheria waaminifu bado wan ashindwa kuwapata.
Umoja na mshikamano:
-Hata hivyo nguvu ya mnyonge ni umoja. Wakazi wa Madongoporomoka wanaapa kuwa fujo hazitasaidia lolote.
Maudhui ya kazi:
Mzee Mago ameifingua kazi ya kuuza vyakula pale katika mkahawa mshenzi katika eneo la Mandongoporomoka.


|