Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Tumbo Lisiloshiba (Said A. Mohammed)

Ufaafu wa anwani “Tumbo Lisiloshiba”

 (7m 43s)
8133 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ufaafu wa anwani “Tumbo Lisiloshiba”
-Hadithi hii imepewa kichwa ambacho kinasadifu yale yaliyomo. Wananchi wa Madongoporomoka walisikia uvumi kwamba kulikuwa na mpango wa kubomoa makao yao ili kutoa nafasi ya upanuzi wa jiji. Walijadiliana mara kwa mara wakiwa katika mkahawa mshenzi wa kiongozi wao Mzee Mago.
-Wakiwa katika mgahawa huo wanaagiza vyakula mbalimbali. Linatokea jitu moja kubwa likatoa agizo kwamba lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine. Lilitishia kwamba wapende wasipende angejitwalia vyakula hivyo.
-Jitu lilikula aina zote za vyakula na kunywa chupa kadhaa za soda. Mwishowe lililipa na kuahidi kwamba lingehitaji chakula mara mbili zaidi kesho yake. Siku iliyofuata, lile jitu litifika kuja 'kula ardhi' ya Madongoporomoka.
- Lile tumbo halishibi si chakula tu, bali rasilimali za raia kama ardhi.
-Tumbo lisiloshiba husimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki — wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kile
kidogo walicho nacho wanyonge. Usasa na maendeleo yameleta ahueni kwa wananchi wachochole au yamezidisha unyanyasaji?


|