Utangulizi wa tumbo lisiloshiba
Answer Text: TUMBO LISILOSHIBA Said A. Mohamed-Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong’ono ukaeneza wasiwasi-hofu.- Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vyote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake ili wahjadili juu ya haki zao za kuishi pale wana pochagua. Wanahojiana mambo juu ya:-Kustahili kuishi kwa Amani na furaha popote nchini mwao.-Namna ya kuruka vikwazo vya sharia vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.-Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu ili kutatua (mazonge ya sharia)-Baadhi ya wanyonge wanataka wapewe visenti vyao vichache waondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka wabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwanguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa pale Madangoporomoka.- Bi Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote. Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mgahawani kilikuwa tayari na kikaanza kunukia na kuwatamanisha wale waliobarizi hapo. Mara likatokea jitu kubwa nakukaa mle ndani. Jitu hilo liliamuru liletewe chakula chote cha wateja wa mzee Mago. Jitu lilifagia aina zote za vyakula: wali wa nazi, mchuzi, nyama ya kuchoma, kachumbari n.k.-Baada ya kula vyakula vyote vya mgahawani hapo lililipa hela yote kisha likaahidi kuwa kesho tena lingekuja na liandaliwe chakula marambili ya kile kilicholiwa. Alfajiri iliyofuata, polisi wakiwa na mirau na bunduki walikuwa wanalinda askari wa baraza la mji wakiviporomosha vibanda vyote. -Kulikuwa na mahangaiko ya wanyonge, wasiwasi na hatan. Kumbe kile kitendawili cha jitu kilimaanisha kuwa ardhi yao ingetwaliwa yote.- Hata hivyo, wanyonge wanashikilia msimamo wao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katika ardhi yao.