Wahusika na sifa zao katika Tumbo Lisiloshiba
Answer Text: Wahusika na sifa zao katika “Tumbo Lisiloshiba”(a) Mzee Mago-Mpenda haki na mtetezi wa haki: yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia suluhisho-Ni mwenye bidii: shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi. Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.- Ni mshawishi: aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.-Ni mzindushi: aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo.Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa wakubwa n k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.(b) Kabwe-Anapenda ushirikiano. Alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.-Anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.-Ni mpenda amani na haki. Alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa Madongoporomoka.(c) Bi. Suruta-Ni mshauri-Ni hodari katika kutoa hoja kwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.(d) Bi. Fambo-Mwanamke mojawapo wa wanyonge.-Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.-Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.(e ) Jitu Ia miraba mine-Ni mkubwa wa kimo: yeye alikuwa pandikizi la jitu Alipoingia katika mgahawa mshenzi wateja wote waligutuka.-Ni mlafi: alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwepo katika mgahawa wa Mzee Mago na kurudia mara tano kabla ya kushiba. Aidha alikunywa soda nyingi sana. vyakula vyote na hata hakusaza chochote.-Ni mwenye madaha: Anajishaua na kumwambia Mago kwamba hajakuja kusaidiwa na Mago pale katika mkahawa bali ndiye anamsaidia Mago.-Ni fisadi: Jitu limehusika katika njama ya kuwaangamiza wanamadongoporomoka na kuwaibia ardhi yao