Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya Ndoto ya Mashaka
Answer Text: Mbinu katika hadithi fupi ya “Ndoto ya Mashaka”(a) Kuna matumizi ya nyimbo-Wimbo wa kwanza ni wimbo wa kuhimiza watu wathamani na kula aina duni ya ndizi ambayo inaweza kufaa ikipata mpishi bora. Wimbo wa pili, umenakiliwa kutoka Redio Tanzania. Huu unatumiwa kuonyesha kuwa Waridi alipomwimbia mumewe Mashaka alikuwaanampa kidokezo kuwa anaondoka kurejea kwa wazazi wake.(b) Methali-Baada ya dhiki faraja-Apewaye ndiye aongezwaye-Kitanda usichokilalia huwajui kunguni wake-Jungu kuu halikosi ukoko-Siri ya mtungi iulize kata(c) Tanakali za sauti-Kokoko iikoo-Kwa kwaa-Puu ngwaaa(d) KinayaMzee Rubeya tajiri mtajika wa ukoo wa Mwinyi anamuo bintiye kwa kijana hohehahe.(e)TakririMiguu hiyo mie nitaingia nayo kaburini! Ee miguu gani hii.(f) Jazanda-Kibuyu hakifichi mbegu.-Mashaka anarejelea vile ambavyo siri hazifichiki.(g) Taswira-Kuna taswira ya wanyonge wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa kwa wino uliokoleza-Kifafa cha uzazi kilimpiga dafrau akaanguka chini.-Picha ya mama Mashaka ya kufa ghafla.(h) Tashihisi-Rangi ya urujuani ilichungulia katika nyufa-Kitanda changu cha mayowe kikapiga ukulele.(i) Tashbihi-Zimepotea bilashi kama moshi-kufuriana kama unga uliomwagiwa hamira(j) NdotoBaada ya Waridi kumkimbia Mashaka aliota ndoto, kwamba wanyonge waliandamana wakadai haki zao kwa nguvu, Walisubiri lakini hawakufaulu. Wakaanza tena harakati zao.Wakati huu wakawa wana hasira zaidi na wakazidisha kelele. Pia wakabeba mabango yenye ujumbe mkali zaidi.Mabadiliko yakaanza, na wanyonge wakapata maisha bora.