Maudhui katika hadithi fupi Ndoto ya Mashaka-Ali Abdullah Ali
Answer Text: Maudhui katika hadithi fupi “Ndoto ya Mashaka”-Ali Abdullah Ali(a) Mkosi maishani-Mashaka alikuwa na mkosi tangu alipozaliwa. Wazazi wote walifariki akiwa mchanga. Alipata mlezi ambaye alikuwa fukara. Mashaka aliishi kwa kufanya vibarua ili kumsaidia-Biti Kidebe mlezi wake. Alipomaliza tu chumba chanane mama mlezi akafariki. Mashaka anaoa binti mrembo lakini kutokana na ufukara anamkimbia yeye na watoto saba.(b) UtabakaMwandishi anaangazia suala la utabaka. Anadhihirisha kuwa kuna watu wengi maskini. Ingawaje wanajaribu kupigana nao bado hawajawahi kujinasua. Mwandishi anatoa tathminipana ya chanzo cha umaskini. Anaonyesha kuwa katika mtaa wake wamo maskini wengi.Chumba cha Mashaka kwa mfano kimepakana na cha jirani. Maji ya kuogea yanapita karibu na chumba cha chao. Watu wanaoishi katika mandhari haya ni maskini wa kupindukia.(c) Ukombozi na mabadilikoWasakatonge wanaona kuwa, hali zao zinakatisha tamaa.Wanapanga maandamano ili kujikomboa. Waliandamana huku wanapiga kelele "Tunataka tufe! Bora tufe! Walifikia kauli hii kwa sababu walichoka kusubiri. Waandamanaji wanazidisha kelele.