Muundo wa hadithi Ndoto ya Mashaka-Ali Abdullah Ali
Answer Text: Muundo wa hadithi “Ndoto ya Mashaka”-Ali Abdullah Ali-Hadithi hii ina muundo usio sahili. Kuna sehemu zilizogawanywa kwa vinyota. Kila sehemu inabeba maelezo tofauti. Sehemu ya kwanza inaeleza juu ya Waridi binadamu na waridi ua wakati huo huo. -Katika msuko wa maelezo hayo ameelezea sifa za waridi ua na Waridi binadamu yaani mkewe.-Sehemu hiyo pia inakuwa kama muhtasari wa kisa kizima.-Baada ya kitangulizi hicho msimulizi anaelezea kisa kilichokuwa kimetokea kabla ya sehemu hiyo ya kwanza, iliyotengwa kwa kinyota. Hapa anaeleza usuli wake na mikasa yote iliyomsibu.- Sehemu inayofuatia kwa mtiririko mmoja, inaelezea juu ya ndoa yake ya mkeka.-Baada ya nyota anaelezea maisha ya ndoa yao.- Hadi sehemu inayoonyesha maisha ya ndoa. Usimulizi wa mkewe alivyomkimbia na mashaka yaliyompata unafuata.Sehemu ya mwisho ina kitangulizi au anwani isemayo; 'Siku nyingi tena ' Sehemu hiyo inaonyesha ndoto na mawazo yake aliyokuwa nayo.Ploti ya aina hii huitwa ploti changamano.