Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Muhtasari wa hadithi, ndoto ya mashake -Ali Abdullah Ali

 (13m 2s)
2356 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
NDOTO YA MASHAKA – Ali Abdullah Ali
Muhtasari
-Hadithi hii inaanza kwa kusimulia uzuri wa ua la waridi na umaarufu wake.
-Linapendeza na kunukia vizuri. Ni ua lenye haiba. Waridi linasimamia msichana ambaye Mashaka alimpenda mno. Ua lake la waridi lilikwanyuka kwanyu likachukuliwa na upepo. Hivyo ndio
Waridi wake alivyotoweka siku moja.
Mashaka alikuwa na makuzi ya mashaka kama jina lake.
-Alikuwa na mama mlezi Biti Kidebe, maana wazazi wake wote walifariki Pindi alipozaliwa. Mashaka amekua katika ukata hadi kifo cha Biti
Kidete. Alikuwa wa kufanya vibarua vya kila aina. Yalikuwa makuzi ya tikiti
maji au tango, ya kuponea umande.
-Mashaka aliozwa Waridi kwa kufungishwa ndoa ya mkeka. Hii ndoa, hufungwa kwa kushtukiza, pale wazazi wa binti wanapomfuma binti yao yuko kwa mwanaume. Waridi na Mashaka walikuwa wakipiga gumzo humo chumbani mwa Mashaka. Mlango ukapigwa teke na
-Mzee Rubeya, akaingia akifuatana na shehe. Wakafungishwa ndoa.
Mzee Rubeya kwa kuwa ni mkwasi, aliona aibu binti yake kuozwa na mtu hohehahe. Yeye na familia yake wakakimbilia Yemeni.
-Hali ya Mashaka ya ukata ilizidi. Waliishi chumba kimoja na watu tisa! Yeye mkewe na watoto saba. Mandhari hayo yalikuwa duni.
Walikaa karibu na choo ambacho hufurika mvua inaponyesha.
-Mabinti walibanana kwenye kitanda kidogo na wavulana walilowea kwa jirani. Mwenyewe Mashaka ni mlinzi wa ZWS.
Mashaka aliwaza na kuwazua akatathmini na kutafuta idadi ya
-Mashaka Tandale alikoishi na kwingine duniani 'Kuna Tandale ngapi Kenya, kuna Tandale ngapi Uganda kuna akina Mashaka wangapi Afrika nzima.
Anashangaa kwa nini jamii za kimataifa hazitaki kuukemea mfumo huu. Mashaka alijituliza na kujiasa kuwa awe na subira.
- Hata hivyo hakusaidika. Katika hali ya kimawazo na kuota baada ya karne moja, Waridi ua lake lilimrudia, akaufurahia uzuri wake na harufu.
- Kabla ya hapo kulikuwa na maandamano makubwa ya wanyonge. Wasakatonge waliandamana 'Tunataka tufe! Bora tufe! Walibeba mabango na kupiga kelele zilizofika kila mahali. Kelele zao zilipenya kama radi kwa watu wa matabaka ya juu.


|