Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Ndoto ya mashaka (Ali Abdulla Ali)

Ufaafu wa anwani Ndoto ya Mashaka

 (6m 20s)
5506 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ufaafu wa anwani “Ndoto ya Mashaka”
-Anwani ya hadithi hii ni Ndoto ya Mashaka. maana mhusika mkuu anaitwa Mashaka. Naye alipatwa na mashaka anuwai. alifariki Mashaka alipomaliza chumba cha nane.
- Mashaka anaozwa binti wa tajiri Mzee Rubeya alipogundua kuwa wanapendana. Ndoa yenyewe ya mashaka.
- Shehe na Mzee Rubeya waliwafuata Waridi na Mashaka walipokuwa wanapiga gumzo chumbani na kuwafungisha ndoa.
-Ndoa hii ilileta aibu kwa familia ya Rubeya na wakahamia Yemeni alikotoka.
-Mashaka alipata watoto saba. Ufukara ukazidi kipimo.
-Waliishi katika chumba kimoja kile kibovu. Shida ziliposhamiri mkewe alitoroka na watoto wake.
- Mara nyingi aliota ndoto ya kuwa Waridi ua lake limerudi, lakini ndoto ikiisha anajikuta yuko pweke kwa mashaka yake. Kisa hiki kinasadifu kuitwa 'Ndoto ya Mashaka '


|