Mhusika Mashaka na sifa zake katika hadithi “Ndoto ya Mashaka”
Answer Text: Mhusika Mashaka katika hadithi “Ndoto ya Mashaka”Kama lilivyo jina lake alikuwa na maisha ya mashaka. Ni yatima aliyelelewa na Biti Kidebe mwenye roho nzuri lakini mnyonge.Sifa za MashakaAlikuwa na bidii: alifanya vibarua vya kila namnakumkimu binti Kidebe mama mlezi.-Ni maskini: alizaliwa katika ufukara na juhudi zake za kujitoa hazikufua dafu.-Ana mapenzi ya dhati: aliwapenda watoto na mke wake, wanapomkimbia anasononeka.-Mwota ndoto: mawazo yake na subira kuhusu kujinasuakutoka makucha ya ufukara yanamfanya daima aote ndoto.-Ana nyota ya jaha: alibahatika kupendana na binti mkwasi na wakafungishwa ndoa. Hata hivyo familia hiyo haikuwa saidia wakaendelea kusalia katika ulitima.-Mwenye majuto: anajutia hali yake ya ufukara na kutamani angeweza kupata suluhisho la kudumu.