Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Shibe inatumaliza (Salma Omar Hamad)

Mbinu katika hadithi fupi ya Shibe Inatumaliza-Salma Omar Hamad

 (6m 58s)
4362 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi fupi ya “Shibe Inatumaliza-Salma Omar Hamad
(a) Nyimbo
-Kuna nyimbo tatu zilizoangaziwa katika hadithi hii. Nyimbo hizi ni za dhihaka na kejeli.Wimbo wa kwanza unachezwa mara kwa mara Mzee Mambo anapokuwa ana sherehe. Wimbo huu ni wa kufumba watu macho kuhusu chanzo cha mali ya Mzee Mambo inayotumika kiholela.
Ujumbe wa nyimbo ni kwamba Mola ndiye anayempatia mja mali yule anayemtaka. Na mtu akishapewa mali yake hawezi akanyang'anywa.
-Ubeti wa shairi unasikika baada ya Sasa na Mbura kula na kuwa katika usingizi wa mang'amumang'amu " Ujumbe wa ubeti huu ni kwamba watu wakishalemewa na dhuluma za wakubwa
itabidi waanze kudai haki zao "
-Wimbo wa tatu nao umejaa kejeli vilevile. Unabainisha wazi 'majuju'- watu wa hadhi ya Mzee Mambo kwamba hawajali lawama zinazotolewa na watu kuhusu vitendo vyao.
(b) Tashbihi
Matumbo yao matupu yakishindana kunguruma kama radi.
(c ) Takriri
Huiga kwa jamii, huiga, huiga.
(d)Utohozi
Obesiti, wesapu, fesibuku, stepu.


|