Maudhui makuu katika hadithi Shibe Inatumaliza
Answer Text: Maudhui makuu katika hadithi “Shibe Inatumaliza”(a) Unyakuzi wa mali ya umma-Kuna unyakuzi unaofanywa na viongozi mbalimbali. Kwa mfano Mzee Mambo ana cheo ambacho hakina wadhifa wowote serikalini. Hata hivyo yeye anajichukulia ujira au mshahara wa kiwango cha juu mno.-Fedha na mali za serikali zinatumiwa na wakubwa kwa shughuli duni zisizo na maana. Mzee Mambo anafanya sherehe kubwa mno kwa sababu kifungua mimba ameingia 'nasari skuli'(b) Ubadhirifu wa mali-Mali ya umma inatumiwa ovyo ovyo na hakuna anayejali. Magari ya serikali hubeba mapambo, maji na kadhalika.-Huingia na kutoka kumshughulikia mtu mmoja. Vyakula vinavyoliwa na vinywaji ni vingi mno.(c) Mapuuza ya viongozi-Makosa yote yanayotendwa na wakuu ya kuharibu mali yanapuuziwa 'sijali lawama'. Hata watu waumie kwa kiasi gani wao hawajali. Viongoziwengine badala ya kuchukua hatua zifaazo dhidi ya wanyakuzi wanangojea wakati muafaka ili nao wanyakue. Pindi wapatapo nafasi hutumia mwendo wa kasi kujinyakulia na kulimbikiza "Na sisi twende tusogee kule " jungu lile linateremshwa.(d)Ukandamizaji wa WanyongeKatika taifa la Mzee Mambo, wachochole hukandamizwa kwa njia nyingi.-Wao wana dhiki na ufukara.-Hulazimika kulipia huduma zote muhimu.-Wakubwa wanadai kuwa wanakula kwa niaba ya wanyonge.