Muhtasari wa shibe inatumaliza-Salma Omar Hamad
Answer Text: SHIBE INATUMALIZA — Salma Omar HamadMuhtasari-Ni kisa kinachohusisha Mzee Mambo ambaye ni waziri kivuli wa wizara zote. Yeye mwenyewe anakiri kwamba hana kazi yoyote.Hivyo yeye ameamua kutumia fursa hiyo ili kujishibisha, "...Mimi nipo kuongeza idadi ya walaji karamuni "-Jambo linalodhihirika wazi ni kwamba katika taifa Ia Mzee Mambo, hakuna uwajibikaji. Fedha za umma hutumiwa kiholela.Kinachotazamwa zaidi ni kuenda kazini na si kufanya kazi-Mzee Mambo hupakua mshahara yaani hujitwalia yeye mwenyewe.Yeye hapewi mshahara.Baada ya kujipakulia mshahara, sasa kunakusherehekea,kuna shangwe, hoihoi na nderemo. Mzee Mambo anapokuwa na sherehe kuna wimbo unaopigwa daima. Wimbo wenyewe una fumbo ndani yake.-Wimbo huu unaonekana kukejeli wale wasio na vyeo. Wimbo huu unaonesha Mzee Mambo kashiba shibe kweli. Hii ni sherehe ya kusherehekea mtoto wake wakwanza kuingia Shule ya chekechea.Sherehe hiyo inarushwa moja meia kwenye televisheni ya Taifa. Aidha, inasambazwa kwenye mitandao Mingine yote ya mawasiliano.Katika sherehe ya Mzee Mambo, magari ya serikali yalipewa m: majukumu mengi; kuleta maji, mapambo, ikibidi kupeleka watoto.Wakati huu watu wanakula vyakula mbalimbali ingawa hakuna kupika. Kuna vyakula vya kubwakia, kutafuna n k.-Wakati wa mchana Sasa na Mbura walipata fursa ya kula vyakula.-Wakati muafaka walioungoja Sasa na Mbura unafika na wao wakajiunga kwenye foleni na kula kupita kiasi.-Kutokana na shibe kubwa sasa anakumbuka shairi ambalo hnabainisha kwamba wale walalao wataamka baada ya kupata matatizo mbalimbali. Wakati huu wote matukio yanarushwa hewani.-Kuna Wimbo wa kejeli ambao waporaji wa mali ya umma. Hawajali hata wakilaumiwa. Yeye anaomba kuishi kwa amani na watu.Shibe waliyokuwa nayo Sasa na Mbura ziliwapa usingizi mzito.Wakagundua kwamba kula kunatumaliza.