TUTORKE TRIAL EXAMINATIONS
STD 8 KISWAHILI LUGHA. TERM 3 2022
Jaza nafasi 1-15 kwa vihasho sahihi
Utunzaji bora wa mazingira ni jambo __1____ katika maisha ya ___2____. Hii ni ____3 ____ kila kiumbe hutegemea mazingira kuishi ____4____ kabisa sisi ____5____ tutaangamia.
Sehemu muhimu ya mazingira ni misitu. Misitu ____6____ manufaa ____7____. Kwanza misitu ____8____ mawingu ya mvua. Mvua ____9____ wasaidia wakulima kupata mazao ya kuyajaza ____10 ____ yao. Misitu pia ni ____11____ ya wanyama. Wanyama hawa wavutia ____12____ ambao huleta fedha za kigeni.
Misitu pia huwa vianzio au chemichemi za ____13____. Nayo maji ya mito hiyo hutumiwa kunyunyuzia mashamba. Kwenye misitu tunapata ____14____ ambayo hutupa matunda. Aidha ____15____ tunazopata sebuleni kutokana na miti.
A.jizuri B. nzuri C. lizuri D. zuri
A. watu nyote B. watu kamili C. viumbe vyote D. viumbe wote
A. kwa sababu B. kwa minajili C.kwa kuwa D.kwa kawaida
A. yakiaribishwa B. zikiharibiwa C. yakiharibiwa D. ikiharibiwa
A. wote B. nyote C. zote D. sote
A. yana B. ina C. zina D. una
A. mingi B. tele C. mwingi D. nyingi
Huvuta B. huvuvuta C. huvutia D. hufuta
A. jikinyesha B. yakinyesha C. ikinyesha D. likinyesha
A. maghala B. stoo C. Vyumba D. matumbo
A. makaazi B. makazi C. nyumba D. mbuga
A. watu B. wakimbizi C. wananchi D. watalii
A. maji B. mitunda C. mito D. miti
A. matunda B. mitunda C. mti D. kuni
A. samani B. vyombo C. viti D. zamani
___________________________________________________________________________________________
Kutoka swali 16-30 chagua jibu sahihi
16. Chagua jibu lenye nomino zilizo katika ngeli ya I-I pekee
A. Kahawa, fedha
B. Chumvi, chupa
C. Sukari, mvua
D. Mali, chai
17. Katika nyumba yetu tuna vijiko vya
A. Kukula
B. Kula
C. Kukulia
D. Kulia
18. Chagua wingi wa sentensi hii
Nitapangia nyumba yangu leo
A. Watapangia nyumba yangu leo
B. Tutapangia nyumba yetu leo
C. Tutapangia nyumba yetu leo
D. Tutazipangia nyumba zetu leo
19. Bainisha matumizi ya kiambishi KI katika sentensi ifuatayo
Alikaribishwa alipokuja
A. Masharti
B. Wakati
C. Jinsi
D. Mahali
20. Kuku ni kimba ilivyo kasuku kwa
A. Tundu
B. Kiota
C. Susu
D. Zeribu
21. Mshororo wa pili katika ubeti wa shairi huitwaje
A. Mloto
B. Utao
C. Mleo
D. Tathnia
22. Orodha ipi inayoonyesha sauti si ghuna
A. Sh,t,p,f
B. M, ng,w
C. V,j
D. S,h
23. Wakati kuanzia saa sita mchana hadi sa tisa huitwa?
A. Alasiri
B. Adhuhuri
C. Majogoo
D. Machweo
24. Kifa ambacho hutumiwa kufunika chakula huitwaje?
A. Kawa
B. Mkungu
C. Upawa
D. Ungo
25. Ni jibu ipi sahihi ya salamu ifuatayo?
Alamsiki_____
A. Marahaba
B. Salama
C. Binuru
D. Poa
26. Kanusha:
Njoo na mle
A. Njooni na msikule
B. Msije wala msile
C. Msije na msile
D. Msikuje na msikule
27. Tunasema roboto la pamba, shehena ni ya
A. Mizigo
B. Magari
C. Sahani
D. Ndege
28. Kamilisha methali:
Kosa moja haliachishi
A. Mke B. mtoto
C. mwingi D. mhalifu
29. Akisami 5/9 huandikwaje kwa maneno?
A. Humusi tisa
B. Humusi tano
C. Tusui tano
D. Tusui tisa
30. Kipi ni kitenzi kilichoundwa kutokana na sifa
A. ulegevu - legea
B. mchevu - choka
C. imba - mwaimabji
D. kicheko - ucheshi
Soma kifungu hiki kisha uyajibu maswali 31-40
Bwana Limbuka alikuwa amekuzwa katika mazingira ya kazi nyingi, wazazi wake waliamini kuwa mtu akifunzwa kazi mapema, atakuwa mkakamavu maishani. Kwake Limbuka alichukulia kinyume. Kimoyomoyo alijiambia kuwa akipata kazi na aoe.kisha apate watoto, hatasumbua. Alitia bidii shuleni na akapita mitihani ya viwango vya juu. Baadaye akabahatika kama tende, akavuka mabonde na milima hadi huko ughaibuni kuongezea masomo.
Akiwa bado ana dukuduku lake la hapo awali, aliangalia familia za huko na kuvutiwa, Akathibitisha kuwa makuzi ya kikwao ni kishamba. Akasahau kuwa kisomo cha kijadi alichopewa kilikuwa ndicho chanzo cha ufanisi wake.
Baada ya miak si haba, alirudi kwao, akaoa na kujaliwa na watotowawili, alimwapia mkewe kuwa yey hatthubutu kushikilia makuzi ya kizamani. Hakuelewa kuwa jambo usilolijua ni usiku wa giza. Hapo basi wakawalea watoto kama mayai. Watoto walipoguswa kidogo walishtakia hali kwa wavyele wao, nao waliwabwekea, wachokozi kwa hasira. Watu wakabakia macho tu! Wakamngojea “ msema kweli wa maisha”. Watoto wakaota pembe za kinyati. Kwa kukosa kazi yoyote, waliigiza lolote lile waliloliona katika runinga. Waliropokwa ovyo popote pale bila tahayuri yoyote. Walipokuwa kidogo walianza kunywa pombe, kuvuta sigara na kutumia dawa zingine za kulevya .
Vituko vilipozidi na kuvuka mipaka, walianza kuwadharau na kuwaaibisha wageni maskini waliowatembelea huko kwao. Waliowahi kufika kwa kwa vigari vya supana mkono walichekwa. Hata watoto walishanga walipoona watu wanapanda ‘ matatu’ au “mabasi”. Walipokwenda kuchukuliwa shuleni kwa gari walilopuuza, walijificha na kusema “ hilo ni gari la sokoni, halitufai” walipoingia kwenye maduka , walichagua bidha ghali. Bwana Limbuka na mkewe walikudhi matakwa ya wana wao wakidhani kuwa safi sana hawa. Ni jasiri na werevu. Hawana undani wowote” . hawakukumbuka kuwa kuna yale yanayofaa kusemwa na kuna yale ya kumezea. Maneno mengine huchoma watu moyoni
Watoto wa Limbuka walizidi kudidimia kisimani, shule ikawapiga chenga. Walishindwa mitihani ya kidato cha nne. Katika hali ya kuokoa jahazi lilikuwa likizama, wazazi waliwap mitaji ya kuanzisha biashara. Baada ya muda mfupi mambo yalivurugika. Mali yote yalifujwa kwa kazi kwani buyu ya asali halichovwi mara moja. Hatimaye ukata uliwanyemelea, wakawa maskini hohehahe wasioweza hata kuwasaidia wazazi wao wazee. Walibaki kuwa motto hakuzwi kwa kubwagiwa mapesa na kuengwaengwa.
Anafaa kufunzwa jinsi ya kubali ulimwengu bila kutegemea nundu za wazazi
Mtegemea cha ndugu hufa maskini.
31. Kulingana na aya ya kwanza , ni kweli kuwa:
A. Bwana Limbuka aliwakuza watoto wake katika mazingiza ya kazi nyingi
B. Limbuka alikuwa kinyume na alivyokuzwa
C. Limbuka alifanya kazi alizopewa na wazazi wake bila kupenda
D. Limbuka hakuwa anafanya kazi ya wazazi
32. Kulingana na aya ya pili, mhusika alisahau kuwa.
A. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
B. Mwacha mila ni mtumwa
C. Majuto ni mjukuu huja badaye
D. Motto mleavyo ndivyo akuavyo
33. Kulingana na aya ya nne . maneno yaliyosemwa na watoto wanazungumziwa yalikuwa
A. Ya uongo
B. Ya ukweli
C. Ya kuchoma
D. Ya watu wazima
34. Maneno “jambo usilojua ni usiku wa giza” yametumia fani gani ya lugha
A. Chuku
B. Tashhisi
C. Istiara
D. Tashbihi
35. Watotowanaozungumziwa katika kifungu hiki waliharibika kutokana na jambo hili hasa?
A. Kutorekebishwa na wazazi
B. Kupewa mahitaju yote
C. Wazazi kubwekea wachokozi
D. Kuishi maisha ya kifahari
36. Watoto wa bwana Limbuka walikuwa;
A. Safi,jasiri,werevu,wasiokuwa na undani
B. Waigizaji,wazembe,waropokaji,walanguzi wa dawa za kulevya
C. Waigaji, wasiokuwa na heshima, wezembe,walevi
D. Wakakamavu,wenye bidii, waigaji,werevu
37. Kwa nini watoto wa Bwana Limbuka walishangaa walipoona watu wakipanda ‘matatu’ au ‘mabasi’ ?
A. Haikuwa kawaida matatu na mabasi kuonekana katika eneo hilo
B. Haikuwa kawaida watu kupanda matatu na mabasi kwa eneo hilo
C. Kwa kawaida watoto hao walisafiri jatika magari za kifahari
D. Matatu na mabasi kwa kawaida yalikuwa ya kusafirisha mizigo
38. Kulingana na aya ya mwisho, si kweli kuwa:
A. Watoto wa bwana Limbuka hawakupita mitihani yoyote shuleni
B. Watoto wa bwana Libmuka hawakufika katika chuo kikuu
C. Watoto wa Bwana Limbuka walijaribu kufanya biashara lakini wakashindwa
D. Watoto wa Bwana Limbuka walizunguka huku na huku bila la kufanya
39. Kulingana na kifungu hiki, motto anafaa
A. Kujiepusha na tabia za kuwategemea wazazi wake kwa lolote
B. Kukuzwa kwa kuzingatiwa makuzi yote ya kale
C. Kupewa mwelekeo wa kuzingatia madili yanayokubalika katika jamii
D. Kufunzwa kufnaya kazi nyingi mapema
40 Kifungu hiki kinasisitiza umuhimu wa
A. Kuipenda na kuijali familia
B. Kuzingatiwa malezi bora
C. Kuzingatiwa mila na itikadi za kiafrika
D. Kuwaelimisha watoto
Soma kifungu kifuatcho kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41-50
Namkumbuka Kamanu tangu tukiwa katika shule ya msingi. Yamkini hakuna mwanafunzi ambaye hakumfahamu shuleni humo. Wapo waliomfahamu na unene wa mwili wake. Shule ya msingi ya Lengajuu ilikuwa ya ghorofa. Ungemtambua mara moja kwamba alikuwa akipanda vidato kwa jinsi alivyohema. Huenda waengine nao walimfahamu kwa kuwagota vichwa bure bilashi. Walimu walikuwa na masimulizi yao tofauti. Mwanafunzi asiyekamilisha mazoezi darasani – kamanu. anayevuta mkia katika mtihani si mwingine.
Kamanu hakupenda somo la kwata wala kushiriki michezo yoyote ile. Daima aliketi pembeni na kusingizia maumivu kila tulipoenda kucheza. Ajabu ni kuwa hata hakuishabikia mchezo yenyewe. Alikuwa na marafiki machache sana. Hulka yake iliwafanya wengi wamwambae kama mkoma
Wakati mmoja, Kamanu alithirika kiafya na kulazwa hospitalini kwa takriban mwezi mzima.japo alikuwa hazidishi hapunguzi, kukosekana kwake kulitutia baadhi yetu kiwewe. Tukahofu kuwa huenda lilikuwa limemsibu jambo baya. Tulisikitika zaidi tuliposikia kwamba alikuwa amelazwa hospitalini. Si wa uji si wa maji. Naikumbuka siku mwalimu wetu alipopanga tumzuru hospitalini. Kwa mara ya kwanza Kamanu alidondokwa na machozi ya furaha. Labda hakutarajia kutuona hasa akizingatia jinsi alivyotudhulumu shuleni. Lakini chambilecho wahenga, adui wako aangukapo mnyanyue
Aliporejea shuleni baada ya kupata nafuu,Kamanu alibadili dira ya maisha yake kabisa. Badala ya kuzozana na wenzake alionekana akitabasamu aliposhiriki mijadara ukariri wa mashairi na vilabu mbalimbali. Lililotushangaza zaidi ni kuona jinsi alivyoshiriki michezo kwa ari kuu. Tulianza kumfaa masomoni sasa hakung’ang’ania kuburura mgwisho kama awali. Alikuwa katika nafasi za katikau kwenye orodha ya matokeo. “ vipi, nafasi yako ya nyuma umemwachia nani” tulimwuliza kiutaniutani
“achene hayo” alitujibu kwa tabasamu” nafasi hiyo sikutengewa mimi
Ilidhihirika kuwa Kamanu alikuwa na vipawa anuwai. Walimu wetu walipania kuvikuza vipawa hvi. Walimfanyisha mazoezi mbalimbali ili aimarike. Siha yake nayo ilianza kuwa mufti. Ule unene wake ukayeyuka mithili ya siagi katika kikaango. Alipenda kukimbiakimbia alipopanda vidato. Si ajabu kwamba alijitolea kutumwa majilisini hata wengine tulipolalamikia kukwea vidato vya ghorofa.
Hivi leo nimwonapo Kamanu hukumbuka kwamba hakuna kubwa lisiloshindwa. Ameinuka kuwa mmojawapo wa wanasoka warajika katika taifa hili. Ukwasi wake ni wa kupigiwa mfano.
41. Ni wazi kwamba
A. Kamanu hakuwajibika ipasavyo darasani
B. Walimu walimchukia Kamanu kwa ulegevu wake
C. Wanafunzi wa Lengajuu walipenda kupigana shuleni
D. Walimu ndio waliosimulia mengi kuhusu Kamanu
42. Chagua jibu lilio sahihi
A. Watu walimdunisha Kamanu kwa unene wake
B. Mwandishi ana hakika kwa mba kila mtu anmjua Kamanu
C. Wenyeji wa Lengaju walimfahamu Kamanu kwa sababu tofauti
D. Mismulizi ndiyr aliyehamikiana vyema zaidi na Kamanu
43. Maneno wamwambae kama mkoma yametumia tamathali gani ya usemi
A. Sitiari
B. Kinaya
C. Tashhisi
D. Tahsbihi
44. Wanafunzi walipoenda kushiriki michezo, Kamanu
A. Alibaki darasani akijisomea
B. Alikaa kando kutokana na maradhi
C. Alishabikia michezo pasipo kushiriki
D. Alijitenga nao na kukaa pembeni
45. Kamanu alipolazwa hospitalini.
A. Hakuhudhuria masomo kwa karibu mwezi nzima
B. Mismulizi ndiye aliyesikitika zaidi
C. Walimu waliungana na wa wasiwasi
D. Wanafunzi wote waliingiwa na wasiwasi
46. Kwa nini kamanu alidondokwa na machozi
A. Hakujua maana ya methali adui aangukapo mnyanyue
B. Hakutarajia kutembelewa na wale aliowadhulumu
C. Alihofia kwamba maradhi yangemwangamiza
D. Alifurahi kumwona msimulizi na mwalimu wake
47. Maneno alibadili dira ya maisha yake kabisa yana maana kuwa.
A. Mienendo ya kamanu ilikuwa tofauti aliporejea
B.. Maradhi yalimfanya Kamanu abadilike kimaumbile
C. Alielezwa waziwazi umuhimu wa kushirikiana
D. Ushauri wa marika ulimfanya Kamanu kubadilika
48. Eleza manufaa ya michezo kwa majibu wa kifungu
A. Kujiunga na vilabu, kujua maana ya utani
B. Kuboresha matokeo, kuwaachia wengine nafasi
C. Kuimarisha afya, kumwaachie mtu kiuchumi
D. Kufanikisha uhusiano, kujitenga na watu wabaya
49. Kamanu kujitolea kutumwa majililisini kunaonyesha kuwa;
A. Amekuwa mtilifu kuliko wanafunzi wengine
B. Hapendi kuketi darasani kwa muda mrefu
C. Anajua manufaa ya elimu, si kama wengine
D. Anatamani kufanyisha mwili mazoezi
50. Neno alivyohema kulingana na muktadha lina maana sawa na
A. Alivyochoka
B. Alivyolegea
C. Alivyotweta
D. Alivyohangaika