Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
Class 7 Kiswahili End of Term 3 Examination 2022
Class: Class 7
Subject: Kiswahili
Level: Primary School
Exam Category: Class 7 End Term 3 Exams
Document Type: Pdf
Views: 2771
Downloads: 53
Exam Summary
TUTORKE END TERM TRIAL EXAMINATIONS
STD 7 KISWAHILI LUGHA TERM 3 2022
Jibu maswali 1 mpaka 15
Soma vifungu vifuatavyo, vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi ya yale uliyopewa
Naam, shukrani zangu za __1__ ziwaendee walimu na wanafunzi wote __2__ kufa kupona kujifunza na __3__ Kiswahili kwa __4__ na mali usiku na mchana. Juhudi __5__kama za mchwa wanaojenga kichuguu kwa __6__ zimekiwezesha Kiswahili kupanda na kupanuka kiasi __7__ kufikia ubora na __8__. Hakika penye nia __9__ njia. Nao umoja ni nguvu __10__ ni dhaifu.
__11__ baadhi ya wanafunzi hawapendi michezo. Ni muhimu kukumbuka kuwa michezo __12__ manufaa mengi sana kwao. __13__ kwa kweli michezo __14 __ watoto __15__.
1. A. hati B. bati C. chati D. dhati
2. A. wanaojitoa B. wanaojitolea C. wanaotoana D. wanajitoa
3. A. kukua B. kupinga C. kukuza D. kukiuka
4. A. nguvu B. pesa C. haki D. hali
5. A. yao B. zao C. lao D. chao
6. A. mawe B. tope C. mate D. mchanga
7. A. ya B. cha C. kwa D. la
8. A. kuhaminika B. kutamauka C. kuthaminika D. kudhaminika
9. A. kuna B. pana C. ina D. iko
10. A. utangamano B. utengamano C. utengano D. utangano
11. Hamkani B. maskini C. yamkini D. makini
12. A. zina B. uno C. yana D. ina
13. A. Ama B. Ati C. Bila D. Wala
14. A. huwapea B. huwapa C. hupata D. huwapasha
15. A. fursa B. ruhusa C. ruhusa D. muda
Kutoka swali la 16 -30 jibu swali kulingana na maagizo
16. Ni sentensi ipi inayoonyesha kivumishi kimilikishi?
A. Kiatu hiki ni kipya
B. Kijana mtiifu hupendeza
C. Alifurahi bali hakucheka
D. Dukani kwenu ni kuzuri
17. Iwapo juzi ilikuwa siku ya Ijumaa, mtondo inakuwa siku gani?
A. Jumatatu
B. Jumanne
C. Jumatano
D. Jumapili
18. Ni nini ufupisho wa babu zake?
A. Babake
B. Babuko
C. Babuye
D. Babuze
19. Andika wingi; Ua unapendeza
A. Nyua zinapendeza
B. Maua yanapendeza
C. Ua zinapendeza
D. Maua zinapendeza
20. Kamilisha sentensi
Sikujui ____ alikohamia
A. Kule
B. Wewe
C. Mle
D. Hapo
21. Mtu anayebeba mizigo kwa malipo huitwaje
A. Kuli
B. Hamali
C. Utingo
D. Machenga
22. Kamilisha methali
_______ huwa mwema
A. Mui
B. Mwizi
C. Mchawi
D. Motto
23. Toa jibu mwafaka kwa salamu hii.
Makiwa
A. Binuru
B. Tunayo
C. Alamsiki
D. Inshallah
24. Kanusha
Ungefika mapema ungelimpata daktari
A. Ungalifika mapema ungalimpata daktari
B. Ungelifika mapema ungelimlipata daktari
C. Usingefika mapema usingempata daktari
D. Usingalifika mapema usingalipa daktari
25. Chagua sentensi inayoonyesha matumizi ya po ya wakati
A. Anapochezea pana shimo kubwa
B. Pole pole ndo mwendo
C. Alipokaa ndipo pao
D. Aliponitafuta alinipata sokoni
26. Mtoto wa nyuki ni jana je, mtoto wa chungu huitwaje?
A. Nirihi
B. Kiwavi
C. Kiluwiluwi
D. Kwida
27. Tunasema mweusi kwama makaa, vile vile mwepesi kama
A. Mboga
B. Pea
C. Mawingu
D. Hewa
28. Chombo kinachotumiwa kukunia nazi huitwaje
A. Mbuzi
B. Kata
C. Susu
D. Kifumbu
29. Neno lipi limeambatanishwa na ukubwa wake sahihi
A. Jina – majina
B. Mzigo- zigo
C. Kitabu – kijitabu
D. Mtu – mjitu
30. Kamilisha “ lingana kama____
A. Kinu na mchi
B. Sahani na kawa
C. Kiko na digali
D. Kalamu na karatasi
Soma kifungu kifuatacho kish ujibu maswali 31-40
Teknolojia imeleta mfumo mpya wa maisha kote ulimwenguni. Imekuwa nadra kwa watu wa mataifa kutekeleza kazi zao kivyao. Hii ni kwa sababu mitambo ya tarakilishi imeenea kote na matumizi yake si mapya tena. Hali hii imekuwa msukumo mpya wa maendeleo katika Nyanja mbalimbali za nchi kama vile biashara, uvumbuzi wa bidhaa mpya viwandani na vyombo vya kuonewa fahari katika makazi za watu vikiwemo radio, runinga na majiko
Kweli, dunia nzima imekuwa kijiji tu hivi, mlango wa kwenu unakabiliana na wakwetu na mawasiliano, mapatano na uhusiano huo kuwa bayana zaidi. Kale, watu walichukua muda mrefu kuandikiana nyaraka zilizochukua miezi kadha kufika; siku hizi huduma hii ya shirika la posta na nyingine hapa na pale si kizuizi kikubwa kwa mawasiliano na umuhimu wake umeachiwa uwasilishi wa vifurushi. Watu wengine hutuma ujumbe mfupi kwa rununu. Barua pepe nazo ni nyingine ambazo zimeimarisha mawasiliano hasa kutoka mabara; pasi kuwa na gharama huu kama hapo awali. Kipepesi na mitambo ya umeme vinatumika katika Nyanja mbalimbali kote duniani
Hata hivyo kila masika yana mbu, nao mbu husambaza malaria. Kupitia vyombo vya habari na mawasiliano, vijana wetu huchukua hulka za kizungu. Matumizi ya dawa za kulevya, kujivalia nusu uchi na lugha chafu ni baadhi ya mambo yanayochangia ongezeko la visa vya ubakaji.
Ni kweli kuwa mambo mapya yakija, watu hujifunza mengi lakini si yote ambayo huja yana manufaa kwetu
31. Watu wa mataifa hawawezi kutekeleza shughuli kivyao kwa sababu __
A. Mawasiliano yamekuwa nag haram kuu
B. Ulimwengu umekuwa kijiji tu
C. Kiwango cha teknolojia kimekuwa sawa kote
D. Mataifa mengine hayana nguvu za umeme
32. Neno nadra kama ilivyotumiwa kwenye kifungu linamaanisha nini
A. Kawaida
B. Muhali
C. Mbeleni
D. Rahisi
33. Ni jambo lipi ambalo limechagua kuunganisha ulimwengu wa sasa
A.Masomo ya sayansi
B.Ueneaji wa nguvu za umeme
C.Uuzaji wa dawa za kulevya
D.Mawasiliano
34. Semi “kuonewa fahari” katika fungu inamaanisha
A.Kukejeliwa
B.Kuchukiza
C.Kujivunia
D.Kubezwa
35. Barua pepe hutumiwa nyakati hizi zifuatazo isipokuwa
A. Zina gharama ya chini
B. Huchukua muuda mfupi kuwasilisha ujumbe
C. Huvumbuzi wa technolojia mpya
D. Watu wote duniani wana elimu ya tarakilishi
36. Shirika la posta na simu ni muhimu hususan katika Nyanja za
A.Barua za watu
B.Vifurushi
C.Matangazo ya bidhaa
D.Elimu ya mawasiliano
37. Kifaa kitumiwacho kutuma nakala na barua katika mashirika ni?
A. Rununu
B. Kipepesi
C. Tarakilishi
D. Kidubwasha
38. Ni methali ipi kati ya hizi inayoeleza kuwa mambo mapya si mabaya kama asemavyo mwandishi
A. Mgeni njoo mwenyeji apone
B. Mwacha mile ni mtumwa
C. Vyote ving’aavyo si adhabu
D. Mlanawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
39. Kulingana na ufahamu, matumizi ya miandarati yanaongeza visa vya
A. Ubakaji
B. Wizi
C. Usalama
D. Uuwaji
40. Kasoro moja ya teknolojia ni
A. Kuelimisha watu
B. Kutangaza habari za ulimwengu
C. Watu kupoteza maadili ya kiasili na kuiga ya kigeni
D. Kueneza habari duniani kote
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Mzaha mzaha hutunga usaha, nao usaha hunuka na una aibu. Aibu nayo huleta majuto na kushuka kwa heshima. Afanyaye jambo lenye aibu haheshimiki
Kwa miaka mingi, wimbo wa uhifadhi wa mazingiza umekuwa vinywani mwa wengi. Kila kukicha tukaelezewa tujiepushe na ukataji ovyo wa miti tukahimizwa na kuelimishwa kuwa iwapo tutaikata miti, basi tupande mingine papo hapo
Tulielezwa tele kuhusiana na utumiaji mbolea asilia ambayo haina madhara katika udongo wetu. Hatukukosa wosia na nasaha kuhusiana na mbinu mwafaka za kilimo ili kuepuka au kuzuia mmomonyoko wa udongo. Lakini yote hayo wengi wetu tuliyatemea mate. Ikawa ni sawa na kumwashia kipofu taa. Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
Tulishauriwa kutoichafua mito yetu lakini tukaigeuza kuwa mabomba ya uchafu. Ni jambo la kusikitisha kuwa na baadhi ya wawekezaji wakielekeza mifereji ya maji taka kutoka viwandani mwao hadi mitoni au maziwani
Si ajabu tena kuona mifereji kutoka viwandani ikielekezwa hadi mitooni, isisaulike maji ya mito hiyo hiyo yanatumiwa na binadamu, mifugo, ndege na wanyama pori
Ukizuru mitaa yetu, yashangaa kuona kuwa nusura katika kila sehemu wazi imegeuzwa kuwa biwi la takataka. Mirundika ya takataka fee imesimama kwa aibu kila mahali. Ni aibu na fedheha yetu hiyo. Kivuli hicho cha fedheha kinatuandama popote tuendapo licha ya kujiita mastarabu na wajuaji.
Matokea ya hayo yote ni masaibu tele yanayotufuata. Hatuwachi kulalamika kutokana na maradhi ya kila aina. Tutaepukaje maradhi ilhali badhi ya mboga tunazotumia hunyunyiziwa maji ya taka taka.
Maradhi yatokanayo na uchafuzi wa hewa limekuwa jambo la kawaida aushini mwetu. Mikurupuko ya ndwele kama vile kipindupindu si jambo geni maishani mwetu. Kweli usaha hunuka. Nayo majuto ni mjukuu mwishowe huja kinyume
Uhaba wa chakula ni tishio kubwa kwetu. Kutokana na mbinu mbovu za kilimo mashamba yetu yanarudi kushindwa kutosheleza mahitaji yetu. Mito yetu nayo inazidi kukauka. Viumbe vya majini vinazidi kudidimia kisa na maana, misitu inazidi kudidimia nayo mito inazidi kuchafuliwa. Mingi yao inaweza kuitwa mito ya sumu.
Maafa hayo yote yanatokana na miaka mingi ya mzaha. Mzaha dhidi ya mazingira yetu. Mambo haya yanastahili kuchukuliwa kwa uzito ufaao. Tukayadharisha. Nayo matokeo ndiyo hayo. Maafa yanayotishia sio tu maisha yetu bali na ya vizazi vijavyo.
Yafaa tuchukue hatua mwafaka imara na za dharura. Tuirejeshe hali ya zamani ili tuweze kufurahia mandhari yetu
41. Kulingana na ufahamu. Majuto hutokana na
A. Mzaha
B. Aibu
C. Kushuka kwa hadhi
D. Usaha
42. Kwa nini mwandishi anafananisha hali husika na kumuwashia kipofu taa?
A. Kipofu hajui faida ya taa
B. Mawaidha yaliyotolwewa wamewajaa watu
C. Mawaidha yaliyotolewa hayakuwanufaisha waliolengwa
D. Mawaidha hayo yalikuwa duni
43. Kulingana na ufahamu mmomonyoko wa udongo husababishwa na?
A. Mvua nyingi
B. Uchafuzi wa mito
C. Utumiaji wa mbolea asilia
D. Njia duni za kilimo
44. Mirundika ya takataka…. Imesimama kwa aibu. Inamaanisha
A. Mazingira yetu machafu inatuaibisha
B. Takataka hizo zinaona aibu
C. Watu wanaona aibu kutupa takataka
D. Takataka nyingi zinahaibisha
45. Kwa nini mwandishi anasema majuto ni mjukuu
A.Uharibifu wa mazingira tuliotekeleza hapo awali unatudhuru leo hii
B. Uharibifu wa mazingira ya leo hii inatuangamiza
C.Tunajutia uajibikaji wetu kwa siku za hapo nyuma
D. Tunazidi kuharibu mazingira licha ya maafa ya jambo hiyo
46. Ukataji ovyo wa miti husababisha ifuatayo ila
A. Mmonyoka wa udongo
B. Ueneaji wa jangwa
C. Uchechefu wa casual
D. Ugonjwa wa kipindu pindu
47. Ni yapi matokeo ya uchafuzi wa mazingira
A. Maradhi, uhaba wa chakula, uchafu na uimarikaji wa uchumi
B. Ndwele, aibu, uchechefu wa chakula na mmomonyoko wa udongo
C. Magonjwa,usaha, ukwaji wa viwanda, vifo vya viumbe na aibu
D. Mmomonyoko wa udongo, vifo vya viumbe, maradhi, kunawiri kwa biashara
48. Tatizo la mazingira linatishia
A. Kutuangamiza sote binadamu
B. Kuangamiza viumbe vyote vya sasa
C. Kuangamiza viumbe vya sasa na vya siku zijazo
D. Kuangamiza tamaduni zetu
49. Mandhari inamaana ya
A. Sherehe
B. Sura ya mahali
C. Matembezi
D. Hali ya hewa
50. Ufahamu huu unatoa ujumbe upi
A. Maafa ya kutohifadhi mazingira
B. Maafa ya mmomonyoko wa udongo
C. Aibu ya usaha
D. Hasara za mzaha
More Examination Papers