Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Class 6 Kiswahili End of Term 3 Examination 2022

Class: Class 6

Subject: Kiswahili

Level: Primary School

Exam Category: Class 6 End Term 3 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 2323     Downloads: 20

Exam Summary


TUTORKE END TERM TRIAL EXAMINATIONS
STD 6 KISWAHILI TERM 3 2022

TIME; 1 HOUR 40MIN

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Msichana wa umri _1_ miaka _2_ alifariki jana katika kaunti ya Marsabit _3_ ya kula mahindi ya msaada kutoka kwa wafadhili. Watu wengine _4_ wa familia yake _5_ ni pamoja na mamake walitibiwa kwa _6_ makali ya tumbo, katika hospitali kuu ya kaunti baada ya _7_ chakula _8_ kilichoshukiwa kuwa na sumu.

“Okech alifariki _9_ ndugu zake watatu walitibiwa kwa maumivu _10_ tumbo” alisema afisa mkuu wa polisi. Mvulana _11_ alifariki mwendo wa saa kumi za asubuhi baada ya yeye na ndugu zake _12_ hospitalini kwa matibabu. Mkuu wa polisi alieleza kwamba wote walikuwa _13_ maumivu _14_ tumbo muda mfupi baada ya kula chakula cha jioni _15_ maumivu hayo yalizidi mchana.
1. A. ya B. wa C. kwa D. na
2. A. mitisa B. tisini C. tisa D. stisa
3. A. badala B. baadaye C. labda D. baada
4. A. watano B. tano C. mbili D. mmoja
5. A. ambamo B. ambao C. ambalo D. ambako
6. A. maumivu B. uchungu C. vindonda D. mateso
7. A. kukula B. kulia C. kulila D. kula
8. A. hiyo B. hilo C. hicho D. huko
9. A. nayo B. nao C. baada D. kabla
10. A. ya B. la C. kwa D. mwa
11. A. huyu B. hawa C. huyo D. hao
12. A. kufika B. kufikiria C. kufikisha D. kufikishwa
13. A. wanalalamika B. wamelalamika C. wakalamika D. watalalamika
14. A. za B. la C. ya D. kwa
15. A. ingawa B. ikawa C. ilikuwa D. itakuwa


16. Sentensi ipi iliyo na matumizi sahihi ya –enye na -enyewe
kitabu chenye ninasoma kina picha chenyewe
mtoto mwenye afya anatembea mwenyewe
maneno yenye ulisema yenyewe nimeyasikia
kwenye uunasomea ni mbali

17. Udogo wa kichwa ni ______
kijikichwa
kakichwa
kijichwa
kijijichwa
18. Mlio mkali wa kufahamishi hali ya hatari kama vile wa gari la wagonjwa au la polisi huitwa ______

kuwika
kubweka
king’ora
kamsa
19. Hili ni umbo gani?
1.PNG


A. B. duara
mraba
C. kopa D. mstatili

20. fupisha maneno haya?
wajomba zako
A. wajombako
B. wajombanu
C. wajombazo
D. mjombazo
21. Ni vazi lipi kati ya haya livalipo na mwanamke pekee?
A. kabuti
B. kanchiri
C. chupi
D. tai
22 Tumia amba ipasavyo
Kipofu ________ tulimwona amerudi
A. ambacho B. Ambaye C. ambako D. aliye
23. Neno jicho liko katika ngeli ipi?
I-ZI B. LI-YA C. A-WA D. LI-YA
24. Nini maana ya semi hii, Chakula alichokipika kilikuwa asali
A. kilikuwa kitamu B. Kilipikwa kwa viungo
C. kilitiwa asali D. Kiliwekwa nyuko
25. chagua neno lifaalo
Yeye ni yatima kwani hana baba ___mama
A. ila B. kama C. wala D. na
26. Andika tarakimu hii kwa maneno 8,659
A. Mia nane mia sita na hamsini na nane
Elfu nane mia tisa hamsini na tisa
Elfu nane mia sita hamsini na sita
Elfu nane mia sita hamsini na tisa

27. tunasema robota la pamba, shehena ni ya
A. udongo B. sahani C. nguo D. mizigo

28. akisami 5/9 huitwa
Tusui tano
Sudusi tano
Subui tisa
Tusui tisa
29. Maamkizi ya asubui ni
A. Alamsiki B. masalkheri
C. Sabalkheri D. binuru
30. Mwindaji haramu katika mbuga za wanyama huitwa?
Jangili
Jambazi
Msasi
msusi
Soma ufahamu huu, kisha ujibu maswali

Nyanya yetu ni mzee sana. Kwa kweli hawezi kufahamu mwaka aliozaliwa, lakini ukimwangalia usoni, utajua mara moja kuwa ana zaidi ya miaka mia moja. Meno yake yote yalihama, nywele zake zimeng’oka na kichwa chake ni kama janga la Sahara.
Kila jioni yeye huwasha moto nje ya nyumba yetu. Nasi wajukuu wake huenda kuota moto pamoja na kupata uhondo wa hadithi zake za kuvutia . zimejaa mafunzo mengi kuhusu heshima, madhara ya uchoyo, wivu, woga, kuwa jasiri na kufanya bidii kazini. Nakumbuka jioni moja nyanya alituhadithia juu ya chui na kobe. Chui alikuwa na tabia ya kumchokoza kobe kila walipokutana kama wasemavyo wahenga kuwa mwenye nguvu mpishe, kobe alivumilia uchokozi wa chui.
Siku moja, chui alimwezeka rafiki yake makofi mpaka akawa hawezi kuvumilia tena. Kobe akawaza na kuwazua jinsi atakanyolipiza kisasi. Mwisho akapata suluhisho.
Kobe alienda katika mzinga wa nyuki na kupata asali kidogo. Alimpelekea rafiki yake chui. Chui alipoionja asali hiyo alitaka aeleze inapopatikana ili aende kuchukua zaidi.
“ Hutaamini hata nikikwambia,” kobe alitamka. Baada ya chui kumbembeleza kwa muda mrefu alimwambia kuwa asali hiiyo ni mavi ya nyani. Kusikia hayo, chui huyo ……..! aliondoka ili aweze kupata asali.
“ Mavi yangu hayatakupendeza hata kidogo,” nyani alimwambia chui. Alimpiga nyani kucha mpaka akanya. Alipoyaonja mavi hayo, alitambua kuwa si matamu kama asali aliyopewa na kobe.. Alipandwa na hasira zaidi akaanza kumtafuta kobe. Ndiposa kobe huficha kichwa chake aonapo mtu akidhani ni chui. Wahenga walinena kobe akiinama anatunga sheria.
31. Umri wa nyanya yetu ni
A. Miaka mia moja
B. Chini ya miaka mia moja
C. Zaidi ya miaka mia moja
D. hatujaambiwa
32. Meno yake yote yamehama ina maana kuwa nyanya yangu ni
A. kibyongo
B. kiwete
C. bubu
D. kibogoyo
33. Lengo kuu la kuwa karibu na nyanya kila jioni ni______
A. kufurahia chakula cha jioni
B. kuota moto
C. kupata hadithi zenye mafunzo
D. kuwashia nyanya moto
34.Neno jingine lenye maana sawa na hadithi ni _________
A ngano B. mafumbo
C. vitendawili D. methali
35. Kulingana na kisa hiki, ni nani aliyekuwa mchokozi
A. kobe
B. nyani
C. chui
D. nyuki
36 Mwisho, kobe alipata suluhisho la.
A. Kulipiza kisasi
B. Kupata asali
C. Kupiga chui makofi
D.Kuvumilia uchokozi
37. “ Hutaamini hata nikikwambia” ni nani aliambiwa maneno haya ______
A. Kobe
B. Chui
C. Nyani
D. nyanya
38. Nyuki hukaa mzingani kama vile mchwa hukaa ______
A. kichuguuni
B. kizimbani
C. zizini
D. kiotani
39 Kobe alilipiza kisasi kwa ____
A. kumpiga chui makofi mazito maito
B. kumdanganya nyani
C. kumpatia chui asali
D. kumdanganya chui
40. Kichwa mwafaka kwa ufahamu hii ni nini
A. Umri ya wazee
B. Umuhimu wa kuzeeka
C. Umuhimu ya kufunzwa hadithi
D. Njia ya kuota moto
Soma habari ifuatayo kasha ujibu maswali 41-50
Hapo kale paka hakukaa katika nyumba za watu. Alikaa mwituni au vichakani tu. Paka alikuwa rafiki wa sungura wa chanda na pete, paka alistaajabia werevu wa rafiki yake. Lakini siku moja mnyama aitwaye funo aligombana na sungura wakapigana hata funo akamuua sungura kwa pembe zake. Paka akawa hana rafiki, akaonelea heri afuatane na huyo funo. Baada ya siku chache wakapambane na chui ambaye alimshika fune akamuua na kumla paka akaingiwa na huzuni akakata shauri kufanya urafiki na chui. Kwa bahati mbaya urafiki huo haukudumu kwa muda mrefu kwa sababu ugomvi ulizuka baina ya chui na simba wakapigana. Katika mapigano hayo akauawa na simba.Paka akafikiri ya kwamba rafiki ambaye angalimfaa sana ni simba. Siku moja tembo alifika pale walipoishi, akachokoza simba kwa maneno makali. Simba akakasirika sana, hapo vita vikali vikaanza. Simba akashindwa na tembo. Paka akasema kuwa rafiki bora ni Yule mshindi mapambanoni. Papo hapo akamwacha simba na kufuatana na tembo. Kabla hawajafika mbali wakakutana na mwindaji aliye kuwa tayari na silaha zake. Bila kuchelewa Yule mwindaji aliyemlenga tembo kwa mshale wa sumu. Maskini tembo akafariki. Paka akamuona mwindaji kuwa rafiki wa dhati.Wakashika safari ya kwenda nyumbani. Mwindaji alipofika nyumbani akalakiwa na mkwe huindo lake na silaha. Paka akaona vile na kuzidi kushangaa. Akadhani kwamba mwanamke ndiye aliyekuwa na nguvu kuliko wote kwa sababu aliweza kumpokonya mwanamme aliyemuua tembo silaha na windolake.
Basi paka akamfanya mwanamke rafikiye na kumfuata kwenda jikoni. Tangu siku hiyo paka huishi nyumbani.
41. Aliyekuwa rafiki mwerevu wa paka ni ____
A. Simba B. Tembo
C. Sungura D. mwanamke
42 Funo alitumia nini kumuua sungura?
A. Kwa kumkatakata
B. Kwa kutumia pembe zake
C. Kwa kumnyonga
D. Kwa kutumia makucha yake
43. Mfuko wa mshale huitwaje?
A. Podo B. Chembe C. Kigumba D. uta
44. Paka alifanya urafiki na wanyama wangapi
A. watatu B. wanne
C. wawili D. watano
45. Paka alifikiria nini alipoona mke wa mwindaji akichukua silaha za mumewe?
A. Kuwa mwanamke ndiye aliyekuwa na nguvu kuliko wanyama wote
B. Kuwa mwanamume amenyang’anywa na mwanamke
C. Kuwa mwanamke alikuwa akitaka kumuua mumewe
D. Mwanamke alinuia kumchoma na kumkatakata
46. Ni mnyama gani aliyemuua chui
A Tembo B.Funo
C.Binadamu D.simba
47. Unafikiri ni kwa nini paka alizoea kuacha marafiki zake
A. alizoea kucheza na marafiki wapya
B. alipendelea rafiki aliyekuwa mshindi katika mapambano
C. alipendelea kuishi pekee
D. alifukuzwa na rafiki zake kwa kukosa ujasiri
48. Mwindaji alitumia _____ kumuua tembo
A.mkuki B.panga
C. mshale wa sumu D.bunduki
49. Methali inayoweza kutumika kueleza kisa hiki ni
A. tama mbale mauti nyuma
B. mla mawe hafi nawe ila mzaliwa nawe
C. akili nywele kila mtu ana zake
D. mwenye nguvu mpishe
50 Kichwa mwafaka cha habari hii ni?
A Paka na mwindaji
B Sababu ya paka kuishi nyumbani
C Paka na mwanamke
D Paka mwerevu





 

More Examination Papers