TUTORKE TRIAL EXAMINATIONS
DARASA LA NANE- MWAKA 2021
KISWAHILI LUGHA
Soma vifungu vifuatacho,vina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo, jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu zaidi
Ulaji wa chakula kinachofaa __1___ kuzingatiwa na kila __2__. Mtu __3__ asipopata chakula chenye virutubishi vinavyofaa anaweza __4___ kutokana na ukosefu wa lishe bora. Lishe bora humsaidia mtu kuepuka ____5__ ya utapiamlo. Ni muhimu kula vyakula vinavyoongeza nguvu, kujenga mwili na vinavyoleta vitamin. Vyakula __6__ huleta vitamin ni kama mboga, maembe, machungwa, tikitimaji na matunda__7__,___8___ mihadarati pia huleta matatizo ya kiafya. Mazoezi nayo__9__ umuhimu wake katika kuimarisha afya. Unashauriwa kufanya mazoezi kila siku ili usipatwe na magonjwa mara kwa mara.
1. A. unastahili B. kinastahili C. inastahili D. wanastahili
2. A. watu B. kimoja C. moja D. mmoja
3. A. yeyote B. yoyote C. mwenye D. wowote
4. A. kugonjeka B. kuugua C. kuungua D. kuteswa
5. A. ugonjwa B. maradhi C. magonjwa D. nduli
6. A. ambavyo B. ambacho C. ambaye D. ambao
7. A. ingineyo B. nyingineyo C. mengineyo D. mingineyo
8. A. kuchukua B. kutumia C. kula D. kunywa
9. A. zina B. ina C.una D. yana
Yohana Jikaze alizaliwa ___10___ familia iliyokuwa maskini __11___. Hata hivyo, ___12__ bali alijikaza kisabuni na kusoma kwa bidii. Wazazi wake walifanya kazi ya utopasi shuleni Harambi. Waliwasili shuleni __13___ asubuhi na mapema na kuchapa kazi hadi ____14___.Bidii hiyo ya wazazi ndiyo iliyoigwa na mtoto wao masomoni, hatimaye Yohana alifaulu katika mitihani. Hapo ndipo wanakijiji wote wakaamini kuwa_____15____
10. A. kwa B. katika C. ndani mwa D. kuwa
11. A. hoe hae B. hahe hohe C. hohe hahe D. hoye hoye
12. A. hakufa moyo B. hakukata kamba C. Hakukanyaga cheleche D. hakufanya juhudi
13. A. hiyo B. penye C. hapo D. hio
14. A. macheo B. mchana C. alfajiri D. magharibi
15. A. umoja ni nguvu utengano ni dhaifu B. mtoto uleavyo ndivyo akuavyo
B. uchungu wa mwana ajuaye ni mzazi D. Bidii hulipa
kutoka swali la16 – 30. chagua jibu sahihi
16. Chagua neno lenye sauti ghuna.
A. chupa
B. Maradhi
C. Thelathini
D. Mshuma
17. Maria akigawa robo mara mbili sawia, alipata akisami gani
A. sudusi
B. Roba mbili
C. Thumni
D. Nusu
18. Sentensi gani sahihi kisarufi?
A. Watume walioleta nyaraka walichelewa kufika
B. Mishumaa yaliyonunuliwa yalitumika yote
C. Mlolongo wa magari yalifuatana
D. Vijana walishambuliwa na viboko maziwani
19. Ni jibu lipi lenye maelezo sahihi?
A. Utaya ni nyama zinazoshika meno kinywani
B. Kipaji ni sehemu ya mbele ya kichwa
C. Kitanga ni sehemu ya vidole
D. Muundi ni sehemu ya mguu iliyo baina ya goti na kiuno
20. Kundi lipi lenye nomina katika Ngeli ya U-U pekee
A. Unga, uteo
B. Umaskini, uyoga
C. Umma, ubavu
D. Uzi,uta
21. Orodha ipi inalingana?
A. tarbia,malenga,ngonjera
B. kibwagizo,vina takhmisa,
C. utenzi, ngonjera,tathlitha
D. ukwapi,utao,manju
22. Chagua sentensi yenye na ya kuonyesha mtendaji
A. anahisi maumivu ya kichwa
B. Susana na Batu ni wanafunzi watiifu
C. Uandishi umefundishwa na mwalimu stadi
D. Mheshimiwa ana gari jipya
23. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo
A. Lo? Nani alikuruhusu kuyanywa maji ambayo hayajachemshwa
B. Lo, nani alikuruhusu kuyanywa maji ambayo hayachemshwa
C. Lo. Nani alikuruhusu kuyanywa maji ambayo hayajachemshwa
D. Lo! Nani alikuruhusu kuyanywa maji ambayo hayajachemshwa
24. chagua viambashi vya nafsi kwenye neno ‘tunakujalia’
A. na-ja
B. li-a
C. tu-ku
D. na-li
25. Ni jibu lipi lenye vielezi pekee?
A. sote,chenyewe,popote,kwenye
B. sana,nadra,safi,vyema
C. kiasi,mno,ajabu,asubua
D. leo,baadaye,laini, laity
26. Kauli:Nekesa na Hadija wameandikishwa insha na mwalimu wao ni Sawa na kusema
A. Nekesa and Hadija wameandika insha kwa niaba yao
B. Mwalimu wao amewaandikia Nekesa na Hadija insha
C. Nekesa na Hadija wameandika insha kwa niaba ya mwalimu wao
D. Mwalimu wao amefanya Nekesa and Hadija kuandika insha
27. Methali “ fimbo ya mbali haiui nyoka” huambiwa anayetegemea walio mbali kutatulia matatizo yake, je asiyejua namna na mikakati bora zaidi ya kutekeleza jambo huambiwa?
A. Makaa hayaoki nyama
B. Kisu kibutu hakichinji kuku
C. Jina la sifa huletwa na matendo
D. Chombo imara hustahimili mawimbi makali
28. Chagua jibu linalounganisha sentensi hizi mbili inavyofaa
Mvua ilinyesha kidindia, Wakulima hawakupanda mapema.
A. Licha ya mvua kunyesha kidindia, wakulima hawakupanda mapema
B. Mvua ilinyesha mapema kidindia la wakulimu hawakupanda mapema
C. Wakulima hawakupanda mapema madhali mvua ilinyesha kidindia
D. Chombo imara hustahimili mawimbi makali
29. chagua jibu lisilolingana na mengine
A. Buda – ajuza
B. Kiambaza – ukuta
C. Panga – pangua
D. Mavyaa – bavyaa
30. Andika katika usemi wa taarifu
“Je, tarakilishi hutumiwa katika mawasiliano?” Mwanafunzi aliuliza.
A. Mwanafunzi aliulizwa ikiwa tarakilishi hutumiwa katika mawasilioni
B. Mwanafunzi alitaka kujua iwapo tarakilishi hutumiwa katika mawasiliano
C. Mwanafunzi aliomba kueleza matumizi ya tarakilishi
D. Mwanafunzi alitaka kujua je, tarakilishi hutumiwa katika mawasiliano
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 31-40
Tuliongoza mifugo yetu hadi malishoni. Ulikuwa ni msimu wa kiangazi nalo jua lilikuwa kali.Sote tulikuwa maghulamu wa hirimu moja.Kiranja wetu alikuwa na umri wa miaka kumi na mitatu.
Baada ya kuichunga mifugo kwa saa mbili hivi,tuliamua kwenda kuogelea katika dimbwi lililokuwa kitalifa kifupa kutoka hapo Machungani. ilibidi tuiache mifugo pale mikononi mwa mmoja wetu. Hakuna aliyejitolea kubaki.Sote tulitaka kwenda kuogelea.
Lisilohudi hubidi. Tulikata shauri kupiga kura. Tulipiga kura na Musa akawa ndiye angeichunga mifugo. Tuling’oa nanga kwa vicheko huku tukimwacha Musa katika hali ya huzuni na upweke.Tulimpa pole za bandia huku tukimcheka kisirisiri. Wengine walisikia wakimtania kuwa wangempeleka maji aogelee malishoni wakati wa kurejea. Laiti tungalijua yaliyotungojea !. Kwa mara ya kwanza nilijigeuza kwa maji yafuatayo mkondo. Niliyatemea mate maonyo ya mamangu.
Tuliandamana na wenzangu moja kwa moja kuelekea dimbwini. Kabla hatujafika, tuliamua kupitia shamba la mzee Kaumu. Konde lake lilijaa mihogo. Tulivamia kwa uroho uliopita ule wa fisi.
Dakika chache badaye, tulikuwa njiani kuelekea dimbwini tayari kuogelea. Ungetusikia ungesamehewa iwapo ungedhani ni kundi la fisi kutokana na vicheko na mbwembwe zetu.
Tulipofika dimbwini na kuanza kuogelea, Kila samaki alitaka kudhihirisha ubingwa wake. Tulipiga mbizi kwa ustadi mkuu. Wengine kama mimi, tulijirushia rushia maji kandokando ya dimbwi. Mtu hujikuna ajipatapo. Au niseme ukimwiga tembo kunya utapasuka msamba. Nilidhamiria kurejea kiamboni nikiwa nzima.
Hata wanagenzi kama mimi, badaye tulitekwa bakunja na uogeleaji. Tulipotanabahi giza lilikuwa likibisha hodi. Mbiombio tulielekea tulipoziweka nguo zetu. La ajabu hata Musa alikuwa kati yetu. Hakuna aliyemwuliza mbona akaja au iliokuwa mifugo kwani maajabu mengine yalitukodolea macho. Nguo zetu hazikuwepo. Mungu mwema! Tuliangaliana bila kusema lolote.
Tukiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, tulisubiri hadi giza lilipotanda kabisa. Kumbuka wahenga walisema usiku ni lebasi bora. Tulifika kiamboni baada ya safari ya tahadhari kuu kupitia vichakani.
Kiamboni nilikuta mengine. Mmiliki wa shamba la mahindi lilipopatikana malishoni alikuwa pale machozi yakimdondoka. Mazao yake yote yalikuwa yameangamizwa na mifugo yetu. Vilevile, Mzee Kaumu alikuwa pale akililia damu yetu. Kumbe alikuwa tayari ameiuza mihogo ile!. Angemwelezaje mteja wake? Yaliyonipata jioni hiyo mikononi mwa mama, sidhani yatafutika akilini mwangu hadi gharighari ya mauti yangu. Kwa njia moja au nyingine yalikuwa ni dira ya maisha yangu. La sivyo hii nisingethaminiwa katika jamii.
31. Kwa nini wahusika walishiriki upigaji kura?
A. walitaka kuenda kuogelea
B. Walikuwa na nia ya kumchagua kiranja
C. Walikuwa wamekosa kukubaliana yupi kati yao angebaki na mifugo
D. Walikosa kiongozi atakayewaongoza
32. Kulingana na ufahamu, ni kweli kusema kuwa.
A. Wahusika wote walifurahia matokeo ya kura
B. Msimulizi hakufurahia matokeo ya kura
C. Wenzake Musa walimtania
D. Kamwe Musa hakuenda kuogelea
33. Tabia ya msimulizi inaweza kujumuishwa kuwa:
A. Utundu na utukutu
B. Utiifu na uwajibikaji
C. Uzembe na mabezo
D. Uaminifu na ukarimu
34. Kulingana na aya tano, si kweli kusema:
A. Musa na wenzake walipitia shamba la mzee Kauma kabla ya kufika dimbwini
B. Msimulizi na wenzake hawakufululiza moja kwa moja hadi dimbwini
C. Wahusika walifurahia uogeleaji
D. Msimulizi na wenzake waliingiwa na tamaa.
35. Kauli “Laiti tungalijua yaliyotungojea” inaweza kujumuishwa kwa methali gani
A. Pili pili isioila yakuwashia nn?
B. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
C. Mzigo u kichwani kwapa latokeani jasho?
D. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza
36. Kulingana na kifungu, mzee Kaumu alichelea nini hasa
A. Mihogo yake kuharibiwa na mifugo
B. Kufidia hasara ya mihogo
C. Kupata hasara ya mihogo
D. Kuwaadhibu msimulizi na wenzake
37. Sentensi “Tulipotanabahi giza lilikuwa likibisha” imetumia fani gani?
A. Msemo
B. Methali
C. Uhaishaji
D. Kinaya
38. Mpangilio upi unaonyesha mfuatano mwafaka wa matukio katika taarifa?
i. Ng’ombe kuangamiza mazao ya mmiliki wa shamba la mahindi
ii. kuliwazia tendo la ukaidi
iii. kupiga kura
iv. Msimulizi kukaidi ushauri wa mama yake
A. iii,iv,i,ii
B. I,ii,iii,iv
C. iv,iii,i,ii
D. ii,iii,iv,i
39. Neno linaloonyesha kutowajibika kwa msimulizi ni:
A. Kuandamana na wenzake malishoni
B. Kujaribu kujifundisha kuogelea
C. Kuamua kupiga kura
D. Kuandamana na wenzake kwenda kuogelea
40. Neno “dira” kama lilivyotumika katika aya ya mwisho linamaanisha:
A. Mustakabali
B. Kifaa cha kuelekeza msafiri
C. Mafunzo
D. Maaarifa.
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 41-50
Makuzi ya watoto hutegemea sana jamii yenye msimamo thabiti katika suala hili.Hoja ya wazazi isiwe tu kujitafutia mali ovyo bali iwe ni ya kutambua warithi wa mali inayosakwa. Hii ndiyo sababu wazazi wengi leo hujikusuru kuisimamisha misingi ya malezi bora kwa watoto kwa kuwasomesha.
Kumsomesha mtoto tu bila msingi wa nidhamu ni kama kulijenga jumba la ghorofa bila msingi imara na kuporomoka kwake si ajabu. Vijana wanapaswa kuelewa umuhimu huu ili wawe tayari kuupokea uongozi na urithi wa jamii.
Misingi madhubuti ya kinidhamu hujengwa tangu watoto wakianza kutambua mambo. Kumngoja hadi mtoto awe mkubwa ndipo aanze kufunzwa maadili ni kama kujaribu kuuwahi udongo ukiwa umekauka na kuwa mkavu; samaki mkunje angali mbichi.
Hapo zamani mambo yalikuwa tofauti. Mtoto aliweza kukosolewa na mtu yeyote hata kama alikuwa mpita- njia. Watoto walikuwa ni wa jamii, hulka zao zilionekana mapema. Watoto walikuwa wakitenda mambo huku wakijihisi kuwa jamii imewakodolea macho
Hisia hizo ziliwafanya kujichunguza, kujikosoa na kutenda mambo kwa tahadhari
Waliheshimu watu wazima bila masharti hali ambayo ilikuza uhusiano bora katika jamii.
Mtoto afunzwaye adabu ipasavyo kawaida hawezi kutetereka popote alipo, iwe shuleni au nyumbani. Mtoto kama huyo kufanywa kuwa bendera inayofuata upepo na watovu wa nidhamu sio rahisi, bali atachukua nafasi ya walimu na wazazi kuyapitisha maadili yafaayo kwa wenzake. Mtoto huyu hukuza mbegu bora katika jamii. Wazazi wakilea watoto wa aina hii na wawaongezee mafunzo huchangia pakubwa katika maendelea ya nchini kwa jumla.
Kuna haja sasa ua kufuata tamaduni na itikadi za kigeni katika maisha. Tukome ubaguzi, uvivu na ubinafsi ili kuwapa watoto mifano bora na miangaza ya kuwakuza kufikiria. kielimu kiuchumi na kitamaduni. Jamii izidishe michango yake katika urekebishaji wa watoto.
Watoto nao wana jukumu la kuyaimarisha maisha yao. Wanapaswa kuziepuka tabia zote mbaya hata kama hawapewi misingi makwao. Wanaweza kuyatupilia mbali maovu ambayo yanazunguka katika jamii. Wakumbuka kuwa urithi bora ule wa kuiga tabia njema, jitihada na kupata elimu yenye manufaa.
41. Kulingana na kifungu, misingi bora ya watoto hukuzwa kwa:
A. Wazazi kutotafuta mali ovyo na kuwasomesha warithi
B. Kuujua umuhimu wao na kuwapa maelekezi
C. Kuwa na Misingi madhubuti shuleni
D. Kufunza watoto kujikusuru kiuchumi
42. Maana ya “ kuporomoka kwake si ajabu ni ni”
A. Haijalishi kuwa ghorofa litaporomoka
B. Malezi ya watoto kuharibika si kazi
C. Wazazi kushindwa na malezi si jambo la kustaajabisha
D. Si vigumu jamii kupoteza warithi
43. Umekauka na kuwa mkavu huweza kulinganishwa na:
A. Madhara ya uchelewashaji wa kufunza nidhamu
B. Ugumu na malezi bora
C. Madhara ya ucheleweshaji wa masomo ya watoto
D. Ugumu wa kuwakosoa watoto
44. Kulingana na ufahamu, watoto wa zamani
A. walikuzwa vigumu
B. Waliwaogopa wazazi wao
C. Walikomaa kwa haraka
D. Walikuzwa kwa ushirikiano
45. Watoto kuhisi kuwa jamii inawakodolea macho, kuliwafanya waweze:
A. Kuithamini jamii zaidi
B. Kuiogopa jamii majumbani
C. Kuwajibika katika jamii
D. Kurekebisha tabia katika jamii
46. Kauli “ … kuwa bendera inayofuata upepo inamaanisha:
A. Mtoto mwenye nidhamu kufuatwa na watovu wa nidhamu
B. Matendo maovu kumfuata mtoto mwenye nidhamu
C. Kawaida ya bendera kufuatana na upepo
D. Mtoto mwenye nidhamu kufuata matendo ya waovu
47. watoto wana jukumu la kuyaimarisha maisha yao. Methali inayoweza kujumuisha kufungu hiki ni:
A. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
B. Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha nina
C. Ukibebwa usilevyelevye miguu
D. Wimbo mui hauimbwi mwana
48. Warithi bora katika jamii hukuzwa kwa:
A. Malezi bora na elimu
B. Kuheshimiwa na wakubwa
C. Malezi ya kizamani
D. Kuaminiwa na jamii
49. Maana ya “ hawezi kutetereka” ni
A. Hawezi kubabaika
B. Hawezi kupotoka
C. Hawezi kushawishika
D. Hawezi kutetemeka
50. Kichwa mwafaka kwa taarifu hii ni:
A. Urithi wa jamii bora
B. Msingi wa jamii bora
C. Majukumu ya malezi
D. Bendera hufuata upepo