TUTORKE TRIAL EXAMINATIONS
DARASA LA SABA- MWAKA 2021
KISWAHILI LUGHA
Soma vifungu vifuatavyo,Vina nafasi 1 mpaka 15. kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo, jaza kila pengo kwa kuchagua jawabu zaidi
Ushirikiano ___1____ ya wanafunzi , walimu na wazazi ni jambo ____2___, ___3___ maanani na wahusika wote . ____4____ huleta mafanikio hasa ya wanafunzi wenyewe . Aidha , hukuza ____5___ya kiheshima . ___6___akabiliwapo na matatizo , hukumbushwa ya wahenga kuwa ___7___kwani wenzake humfaa kwa hali na mali.
1. A . baina B Kati kati C miongoni D kati
2. A. linalohitajika B. inayohitajika C. inaohitajika D. yanayohitajika
3. A.kutia B. kutilia C. kutiliwa D.kutiwa
4. A. hiyo B. huu C. huo D. ule
5. A. maadili B. maarifa C. maoni D. nasaha
6. A .lolote B.yeyote C. yoyote D. wowote
7. A. mazoea yana taabu B. Chanda chema huvishwa pete C. mkataa wengi ni mchawi
D. ndugu mui heri kuwa naye
___8___maisha yangu ya ___9____, taswira ya Mwalimu Busara hunijia. Ndiye aliyechangia katika ___10____ kwangu masomoni ___11___wake katika somo la Kiswahili ulimwezesha kutumia kamusi ipasavyo . Akasisitiza kuwa kati ya maneno : shtaka , somea Sinai na sebule ; linapopatikana la tatu katika kamusi ni ___12____. Katika sarufi , akatubainisha kuwa kutokana na kitenzi ‘vumilia’ tunapata
“uvumilivu” ambalo ni ____13___. Pamoja na ukarimu wake, nilijifunza msemo wa kuwa na ___14____. Kweli , bwana Busara asingalikuwepo ___15___ hayo yote muhimu .
8. A. nikiyakunjua B. nikikunjua C.nikiyakunja D.nikikunjika
9. A . baadaye B. usomi C. leo D.kisogoni
10. A. mafanikio B. fanaka C. kufanikiwa D. ufanisi
11. A. ubunifu B. ustadi C. uungwana D. uzalendo
12. A .Sebule B. sinia C .somea D.shtaka
13. A.nomino B.kitenzi C. kivumishi D.kielezi
14. A. mkono birika B.mkono mzuri C.mkono wazi D. mkono mrefu
15. A. nisingalijifunza B. nisingejifunza C .ningejifunza D. ningalijifunza
kuanzia swali la 16 -30, jibu kulingana na maagizo
16. Nyota wengi ni kwa thurea ilhali , miaka kumi ni kwa ______
A. dasani
B. karne
C. mwongo
D. korija
17. Chagua sentensi ambayo imetumia mtajo
A. “ Upanzi wa miti ni muhimu kwetu sote,” Mwalimu alisema
B. Je, unafahamu tofauti kati ya vitawe na visawe
C. Mbung’o ni mdudu aambukizaye malale
D. Hakika, asiyesikia la mkuu
18. Tambua sentensi iliyotumia kiambishi ‘’PO’’cha wakati
A. hapo mnapolima ndipo mliponunua
B. Waliposimama ni pachafu sana .
C. Palipojengwa nyumba mpya ni pangu
D. Alipoenda alimkuta akisoma
19. Ukilima shamba lako sehemu ndogo kila siku mwishowe shamba kubwa litaisha ,
chagua methali inayokubaliana na maelezo haya.
A. Mkulima ni moja walaji ni wengi
B. Bandu bandu huisha gogo
C. Ukipanda pantosha utavuna pankwisha
D. Mkataa pema pabaya pamwita
20. chagua wingi wa sentensi ifuatayo
Mkokoteni wangu si wa kubebea dawa
A. Mikokoteni yangu si ya kubebea dawa
B. mikokoteni yetu si ya kubebea madawa
C. mikokoteni yangu si ya kubebea dawa
D. mikokoteni yetu si ya kubebea dawa
21. Sentensi ‘mtoto ambaye anacheza ni mzuri’
Itaandikwaje bila kutumia ‘amba – ‘?
A. mtoto anacheza ni mzuri
B. Mtoto amabaye anayecheza ni mzuri
C. Mtoto anayecheza ni mzuri
D. Mtoto ambaye achezaye ni mzuri
22. kamilisha methali hii
Kunguru mwoga hukimbiza ____zake
A. Mkia
B. Kivuli
C. Mbawa
D. Manyoya
23. Kiungo kipi ambacho hakijalinganishwa kwa usahihi na matumizi yake
A. Kibofu – huhifadhi mkojo tumboni
B. moyo – husafisha damu
C. pafu- husafisha hewa
D. ini- huwezesha kiwango cha sukari
24. Tambua ukanusho wa “ ungesoma kwa bidii ungepita mtihani”
A. Usingesoma kwa bidii usingepita mtihani
B. Hungesoma kwa bidii hungepita mtihani
C. Haungesoma kwa bidii haungepita mtihani\
D. Usiposoma kwa bidi hutapita mtihani
25. Nomino gani zinapatikana katika ngeli ya U-I pekee?
A. mitume,mikunge,mijusi
B. miwa,miwani,mkono
C. mikeka,milima,mihogo
D. mti,mkate,mvua
26. Tegua kitendawili Huku ng’o na kule ng’o
A. njaa
B. giza
C. mwizi
D. umaskini
27. Chagua sentensi ambayo ni sahihi kisarufi
A. Maji yale masafi ni ya kunywa
B. Mwanafunzi mgani ambaye alipewa zawadi?
C. Mimi ndiye mwanafunzi bora kuliko wote
D. Sisi sote tunapenda Nchi ya Kenya
28. Nomino “ulinzi” inatokana na kitenzi linda ilhali nomino “ uchezaji inatokana na kitenzi gani?
A. Mchezo
B. cheza
C. michezo
D. mchezaji
29. Jibu gani linaloonyesha neno lenye silabi tatu
A. ufa
B. kiti
C. kitabu
D. fululiza
30. Shairi lenye mishororo mitano huitwaje?
A. Tarbia
B. Ukumi
C. Tathlitha
D. Takhimisa
Soma kifungu kifuatayo kisha ujibu maswali 31-40
Simba na fisi walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana . urafiki wao ulishinda hata uhusiano wa ndugu wa toka nitoke . ulikuwa ule uhusiano wa mmoja anapojikwaa dole , anayeuhisi uchungu hasa ni huyo rafiki . Wenzao porini hawakuisha kuusifu urafiki huu . Hakika hata waliwahimiza watoto wao kuiga mfano wa simba na fisi . Kilichowavutia wanyama zaidi ni tabia ya simba na fisi kuchuma pamoja na kuzipa familia zao mahitaji pamoja .
Hali iliendelea hivyo hadi wakati simba na fisi walipojifungua vitinda mimba wao . Uzazi huu ulisababisha mabadiliko makubwa katika maisha yao ,licha ya uzee uliokuwa umebisha hodi simba na fisi walikuwa na vinywa zaidi vya kulisha .Kadhalika , vitoto hivi vikembe vilihitaji uangalizi zaidi . Visingeweza kuachiwa ndugu zao . Hali hii iliwafanya wasiweze kuandamana usasini . Waliafikiana kupishana zamu katika majukumu yao . Wakati ambapo simba angeenda kuwinda , fisi angebaki nyumbani akiwatunza watoto . Zipo baadhi ya nyakati , japo kwa nadra mno , fisi alipojitolea kwenda kuwinda . Jambo lililomtia simba wahaka ni kwamba kila fisi alipobakia nyumbani , chakula walichokuwa wameifadhi kwa matumizi ya baadaye kiliota mbawa.
Fisi alipoulizwa hakukosa kauli ya kujitetea . ‘’Mambo yamekuwa magumu siku hizi . Ulezi una changamoto zake . kumbuka pia tuna waivu . Kozi amekuja hapa na kutaka kuwanyakua watoto wetu . Ilibidi nipambane kwa jino na ukucha kuwaokoa . Katika hali hii nilisahau kuwa ghala lilikuwa wazi . Hata kitali kilipokwisha , nilitahamaki kuwa ghala ilikuwa tupu , ikawa ni yale ya mwangaza mbili…………,’’akasema fisi .Lile ambalo simba hakujua ni kwamba fisi alikuwa akikiiba chakula kujinufaisha yeye na wazazi wake .
Tabia hii ya fisi iligeuka kuwa ngozi ya mwili .Simba naye alizidi kumshuku fisi .Hata hivyo , alipoendelea kuuliza kuhusu muujiza wa kutoweka kwa chakula fisi alimhadaa kwamba kwa kweli chakula kilikuwa kikichukuliwa na simba jike mwingine aliyekuwa akiishi ziwani . Hili lilimchemsha simba nyongo , akakata shauri kwenda moja kwa moja kukabiliana na adui huyo . Simba alisimama ukingoni mwa ziwa huku akiyatazama maji yaliyotulia kana kwamba yanamwogopa . Mbele yake , ndani ya maji , alimwona simba jike mwenzake aliyefanana naye kama shilingi kwa ya pili . ‘’ Kumbe ni kweli kuwa dada yangu huyu hutuendea kinyume ? kumbe ndiye anayetaka kuutia ufa udugu baina yangu na fisi ? simba alijiuliza .
Simba hakujua vipi lakini alijipata ndani ya ziwa ; hasira imemtuma kupambana na simba jike mwenzake . Alitwaa mafumba yake kumchanachana huyo simba lakini lo! alishangaa kwa nini simba yule alihepa kila alipomtafuta . Haukupita muda mrefu kabla ya simba kuhisi mngato mkali kwenye mguu wake.
Alipotazama alimwona mamba mkubwa ajabu anaendelea kungwafua minofu ya nyama kutoka pajani pake . Alitaka kuangua kilio lakini akajikanya . ‘simba haonyeshi maumivu hata mbele ya matatizo makubwa . Huku kutakuwa kujidhalilisha , ‘simba alijisema . Baadaye alimrukia mamba kwa hamasa kuu, moto wa mapigano ukawaka . mapambano yalipokatika wawili hawa walikuwa wameumia si haba . Simba alikuwa amedhoofika mguu , naye mamba akabaki na kigutu cha mkia . Simba alifika nyumbani akiwa hoi kwa maumivu , majonzi na kukata tamaa . Fisi alipomtazama , michirizi ya machozi ya mamba ilimtiririka kama maji bombani .Alimwendea simba na kutaka kumkumbatia . Hata hivyo , mtazamo wa macho ya simba ulimwonya fisi dhidi ya tendo hili na kumfahamisha fisi kuwa urafiki wao wa miaka na miaka umefikia ukingoni .
31. Maneno “marafiki wa kufa na kuzikana” yanamaanisha kuwa simba na fisi walikuwa marafiki
A. hata baada ya kufa
B. Wa dhati
C. Walioweza kumzika aliyekufa
D. wa kufa kupona
32. Kulingana na aya ya pili , si kweli kuwa
A. Simba na fisi walikuwa na watoto wakubwa kabla ya kujifungua vitindamimba
B. Simba na fisi waligawana majukumu ili kuwalinda wana wao wachanga
C. Baadhi ya nyakati , mara nyingi fisi alijitolea kuwinda
D. Simba na fisi walizijali mno familia zao
33. Kilichowapendeza wanyama wengine porini hasa ni hali ya fisi na simba
A. kuvumilisha hata kama fisi alikuwa akiiba chakula
B. Kushirikiana wakati waliposhambuliwa na adui
C. Kupendana kiwango kwamba mmoja alipojikwaa dole , mwenzake ndiye aliyehisi uchungu
D. Kutafutia chakula pamoja na kuzitunzia familia zao pamoja .
34. Kifungu kinaonyesha kuwa fisi alikuwa na tabia gani ?
A. Mvivu na mwenye tamaa
B. Mwenye tamaa na mjanja
C. Mjanja na mwoga
D. Mwenye tamaa na mwaminifu
35. Mwandishi ana maana gani anaposema kuwa fisi alimhadaa ?
A. Alimdanganya
B. Alimwelekeaza
C. Alimshauri
D. Alimhimiza
36. Methali gani inayoweza kuelezea ujumbe katika aya ya tano ?
A. Simba mwenda pole ndiye mla nyama
B. Tamaa ilimwua fisi
C. Hasira hasara
D. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
37. Mbele yake , ndani ya maji , alimwona simba jike mwenzake aliyefanana naye kama shilingi kwa ya pili . Kauli hii inamaanisha kuwa simba aliona
A. Simba aliyeishi majini
B. Uso wa mamba akadhani ni simba
C. Uso wa fisi aliyekuwa akila chakula
D. Uso wake majini akadhani ni simba mwingine
38. Kwa nini simba hakuangua kilio hata alipoumwa na mamba?
A. Alishindwa kulia akiwa ndani ya maji
B. Mdomo wake ulikuwa umeumwa na mamba
C. Hakutaka kuoneka mnyonge
D. Alijua kuwa kuanza kulia kungemzuia kumshambulia mamba
39. Aya ya mwisho inaonyesha kuwa michirizi ya machozi
A. ilitoka machoni pa mamba kwa maumivu yaliyoletwa na simba
B. ilionyesha huzuni na hali ya fisi kumhurumia rafiki yake .
C. Ilikuwa ya uongo kutoka kwa fisi kwani hakumhurumia wala kumjali simba
D. ilitoka machoni pa simba kuonyesha maumivu , majonzi na kukata tamaa
40. Urafiki wa simba na fisi ulifikishwa ukingoni na
A. Unafiki wa fisi
B. ujinga wa simba
C. Ukatili wa mamba
D. Fitina ya wanyama wengine
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Michezo ni mojawapo ya vitu ambavyo huwafurahisha mno watoto . Si ajabu kupata baadhi ya watoto hupendelea kucheza kushinda kula .Jambo la kimsingi ambalo watoto hao hufahamu na kuzingatia ni furaha iletwayo na michezo hiyo . Wao hupenda kucheza wakiwa na nia na azma moja tu ya kujifurahisha .Mara kwa mara utawapata watoto wakicheza kwa furaha chungu nzima na kucheka kwakwakwa kama manyani . Hata hivyo michezo baina ya watoto ina manufaa mengine tele . Ingawa watoto wenyewe huenda hawafahamu manufaa hayo , ni vizuri wapewa fursa ya kucheza ili wanufaike Zaidi.
Michezo huwasaidia watoto kuimarika kiafya . watoto wanapocheza, mifupa yao hufanyishwa mazoezi na kuzidi kuwa imara. Michezo mingi ya watoto huhusisha kukimbia hapa na pale , kubebana na pengine kubeba vitu kama vile mawe madogo .Mtoto anayecheza mara kwa mara mifupa yake huwa migumu na hivyo si rahisi kuvunjika . Aidha wakati wa kucheza kwa watoto damu huweza kusambazwa mwilini kwa kasi na hivyo kudumisha afya ya moyo .Akili ya mtoto hufanya kazi kwa kasi sana wanapocheza ili kuamua mahali pa kujificha ili asipatikane kwa urahisi au kuuhepesha mpira kwa haraka. Hali hii pia huchangia kuboreka kwa afya ya akili.Baada ya kucheza,mtoto huhisi utulivumkubwa wa akili.Yeye huweza kulala fofofo na kwa utulivu mkubwa.
Isitoshe,michezo ya watoto hujenga lugha yao. Watoto wanapoanza kucheza, wengi wao huwa hawafahamu msamiati mwingi.Kadri wanavyozidi kucheza, ndivyo wanavyofahamu maneno zaidi ya lugha husika. Utagundua kuwa mtoto ambaye pengine alijua maneno machache tu anajikaza kidogokidogo tu na baadaye atafahamu maneno chungu nzima ya lugha hiyo. Aidha, imetokea mara si haba kuwa mtoto ambaye hakufahamu lugha yoyote anapowekwa na watoto wenzake wanaofahamu lugha hiyo, yeye hujifunza lugha hiyo. Nyakati nyingine ni vigumu kujua kuwa mtoto huyo anajifunza. Hii ni kwa sababu mtoto huyo huweza kujifunza neno moja tu au mawili kwa siku. Mtu hutokea kupigwa na butwaa anapong’amua kuwa mtoto amejifunza maneno mapya au lugha mpya.
Kadhalika, ubunifu wa mtoto huimarika mno kutokana na michezo hiyo yao.Ukiangalia kwa makini watoto wanapocheza utagundua kuwa watoto wenyewe ndio ambao hubuni michezo. Wakati mwingine utashangazwa namna walijiundia michezo hiyo. “Ni nani aliyeamua kuwa mchezo huu huchezwa na watu watatu au wanne? Muda wa mchezo huu uliamuliwa na nani?Ni nani aliyejua mbinu ya kumjua mshindi katika mchezo huu? Sheria za mchezo huu ziliundwa na nani?”Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo humsumbua mtu.
Hatimaye, mchango mwingine wa michezo hii katika maisha ya watoto ni kuimarisha maadili.Watoto hujifunza kuwana heshima kwa sharia za nyumbani,shuleni nan chi kote kupitia michezo. Kila michezo huwa na sheria zake. Yule asiyetii sheria hizo hupewa adhabu mbalimbali kama vile kupoteza alama,kuondolewa katika mchezo na adhabu zingine.Kupitia njia hii, watoto wanapocheza hujikaza kisabuni ili wafuate sheria hizo. Polepole, mtoto hujua kufuata sheria . Umoja nao huimarika kwa kuwa watoto walio katika timu moja hulazimika kucheza kwa pamoja kama kikundi ili kujinyakulia ushindi.
Ni vizuri kutenga wakati wa kucheza ikiwezekana kila siku. Hata hivyo tusicheze kila wakati. Tuhakikishe kuwa hatusahau mambo mengine kama masomo au kutangamana.
41. kulingana na aya ya kwanza , ni kweli kuwa
A. Michezo ndicho kitu cha pekee kiwafurahishacho watoto
B. watoto wote hupendelea kucheza kushinda kula
C. kupata baadhi ya watoto wakipendelea kucheza kushinda kula hushangaza
D. sababu ya pekee ifanyayo watoto wapende kucheza na kupata burudani na furaha
42. Maneno “ Kucheka kwakwakwa kama manyani “ yametumia fani mbili za lugha. zitambue
A. tashbihi. sitiari
B. nahau,sitiari
C. tanakali, tashbihi
D. nahau, nakali
43. Gani si manufaa ya michezo kwa mtoto kulingana na haya ya pili
A. huchangamsha na kufurahisha mtoto
B. Husababisha utulivu mkubwa kwa akili
C. Huimarisha afya ya moyo
D. Hufanya mifupa iwe imara na yenye nguvu
44. Michezo mingi ya watoto huhusisha
A. kujificha, kutafutana,kucheza kandanda
B. kukimbia,kubebana,kubeba mawe madogo
C. kuhepesha mpira, kubebana, kubeba mawe mengi
D. kuruka kamba,kujificha,kubeba mawe madogo
45. Nini ambacho humletea mtoto usingizi mzito
A. uchovu wa mwili
B. maumivu ya viungo
C. utulivu wa akili
D. kucheza mingi
46. Maneno kupigwa na butwaa yana maana gani jinsi yalivyotumika katika kifungu?
A. kufahamu
B. kushangaa
C. kufurahi
D. kushtuka
47. Ujumbe katika aya ya tatu unaweza kurejelewa kwa methali gani?
A. Mcheza kwao hutuzwa
B. Haba na haba hujaza kibaba
C. Ngoja ngoja huumiza matumbo
D. Ngoma ya wana haikeshi
48. Maswali ambayo mtu hujiuliza kuhusu mchezo iliyobuniwa na watoto huhusu mambo yafuatayo isipokuwa
A. Idadi ya wachezaji
B. muda wa kucheza
C. umuhimu wa kucheza
D. sharia za mchezo
49. Michezo ya watoto huimarisha ubunifu kwa kuwa
A. Michezo hiyo humsaidia mtoto kuwa na afya bora
B. michezo hiyo humsaidia mtoto kubuni lugha mpya
C. michezo husaidia mtoto kuchezea katika mazingira ya furaha
D. michezo hiyo hutungwa na watoto wenyewe
50. Aya ya tano inaonyesha kuwa michezo hujenga nini miongoni mwa watoto
A. utiifu,ushirikiano
B. ubunifu,sharia
C. sharia,umoja
D. ubunifu, utiifu