Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Class 6 Kiswahili End of Term 2 Exams 2021

Class: Class 6

Subject: Kiswahili

Level: Primary School

Exam Category: Class 6 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1641     Downloads: 14

Exam Summary


TUTORKE TRIAL EXAMINATION
DARASA LA SITA – MUHULA WA PILI – 2021
KISWAHILI LUGHA
SOMA MAAGIZO YAFUATAYO
1. Tumia penseli ya kawaida
2. Hakikisha ya kwamba yafuatayo umeandika katika karatasi ya majibu
a) Jina lako b) Jina la shule yako
chagua jibu sahihi kujaza nafasi zilizoachwa wazi kuanzia 1- 5
Mgeni wa____1___ alipendezwa sana kumwona___2____ mwenye moyo wa kupenda ___3____ wakati wa kutoa___4 ___ kwa washindi ulipofika Juma alipata zawadi __5___. Vikiwemo ___6___ vidigi vidogo na hata au cheti cha michezo.
Aliahidi kumlipa Juma __7___ ya shule ya____8____ kama angalipata mtihani wa KCPE na kama asingepata vyema,yeye angemsaidia apate_____9____ambayo ingemsaidia katika __10___ yake.
Alitaka mwalimu wake wa ___11__ amjulishe __12__ tu matokeo ya mtihani yatakapo ____13____.Baada ya michezo wanafunzi wote wali____14__ Juma kwa __15__ wake.
1. A. heshima B. kuogofya C. hofu D. busara
2. A. mwizi B. kijana C. mlevi D. mvuvi
3. A. chokozi B. kijana C. michezo D. fitina
4. A. zawadi B. vipeo C. shukrani D. heshima
5. A. chache B. ufinyo C. kochokocho D. mpwitompwito
6. A. uma B.sahani C. Jembe D. vikombe
7. A. nauli B.kiingilio C. hongo D. karo
8. A. vidudu B. visiwi C. upili D. msingi
9. A.kazi B. bazi C. koti D. fidia
10. A. raha B. maisha C. wizi D. daraja
11. A. dunia B. kanisa C. darasa D.daraja
12. A. muda B. pindi C.ghafla D. kabla
13. A. imbwa B. nenwa C. tangazwa D. lalamika
14. A. msifu B. mtusi C. mcheka D. mkemea
15. A. uvumilivu B. ushenzi C. upole D. ubingwa

kutoka swali a 16-30, jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa
16. Tusui tatu ni ____
A. 3/5
B. 3/8
C. 3/9
D. 3/10
17. Mtoto huyu ni _____
A. safi
B. wasafi
C. msafi
D. usafi
18. Eleza maana ya msemo huu;
Kupiga soga
A. kuogelea
B. kuongea
C. kuongelea
D. kuongelesha

19. Shairi la michororo mitano huitwaje?
A. Tarbia
B. Ukumi
C. Tathlitha
D. Takhimisa
20. Tegua kitendawili
Ubwabwa mtamu wa mwana
A. nanasi
B. yai
C. usingizi
D. jua
21. Kanusha
Baba amefika nyumbani.
A. Baba hakufika Nyumbani
B. Baba hajafika nyumbani
C. Baba hafikangi nyumbani
D. Baba hatafika nyumbani
22. Makao ya ndege huitwa
A. kizimba
B. tagio
C. zizi
D. kiota
23. Dada wa mama yako utamwitaje?
A. shangazi
B. halati
C. mwanyumba
D. ami
24. Kamilisha methali hii
Kunguru mwoga hukimbiza ___ zake
A. mkia
B. kivuli
C. mbawa
D. manyoya
25. Mkusanyiko wa wachawi wengi huitwa
A. umati wa wachawi
B. kilinge cha wachawi
C. masongamano wa wachawi
D. biwi la wachawi
26. Mahali maalum pa kufanyia vipimo na utafiti katika hospitali ni.
A. thieta
B. maabara
C. wadi
D. maktaba
27. Kitabu ____ kitafaa kwa kusoma
A. yeyote
B. wowote
C. lolote
D. chochote
28. Andika kwa wingi
Mwalimu wangu hutumia karatasi
A. walimu wetu hutumia karatasi
B. walimu wangu hutumia makaratasi
C. Walimu wangu hutumia karatasi
D. Walimu wetu hutumia makaratasi
29. Ni maneno yapi ambayo yote ni viunganishi
A. jia,ingawa,lakini,madamu
B. hawa,wale,sawa,vyema
C. ila,kwa sababu,juu,swadakta
D. japokuwa,iwapo,zuri,ingawa
30. Mtoto alipolia nilijaribu kumtuliza na?
A. kumposha
B. kumpoza
C. kumponza
D. kumpoesha



Soma ufahamu huu kisha ujibu maswali 31-40
Katika nchi moja palizuka ugonjwa wa ajabu ambao uliwaua wanyama na watu bila kuchagua. Basi wakazi wa sehemu hiyo waliamua kutafuta dawa au tiba ya ugonjwa huu kwani ilikuwa wazi wote wangemalizwa na ugonjwa huu. Basi walikwenda kwa waganga wakawaita kuja kuwatibu kabla hawajakata roho.
Waganga walijaribu lakini hawakufaulu wala kufua dafu, wakaenda katika mataifa ya mbali kutafuta angalau daktari ambaye angeweza kuutibu ugonjwa huu lakini hawakupata hata mmoja. Watu walioishi katika nchi hii walikuwa wamefanya makosa mengi na dhambi nyingi. Kwanza watu hawa walikata kabisa kutofanya mabo waliyokatwa na wazee wao. Watoto wao hawakujali lolote. waliwatusi wakubwa na wakazkosa kufanya walivyoambiwa. Vijana wote hakuna aliyetaka kupata elimu. Walisema elimu na upuuzi mtupu.
Basi kwa sababu ya mienendo mibaya adhabu iliwashukia. Alikuwpo mzee mmoja aliyekula chumvi nyingi sana aliyeishi pamoja na mjukuu waked mbali kabisa katika pori. Mzee huyu alikuwa Nabii wa Nchi hii.
Watu wote walimsahau na hawakushauri kwa lolote. Kumbe haikukubaliwa kwa hizi sharia na nyingine nyingi ndipo maradhi yakawapata. Watu waliendelea kufa hadi wakabaki wachache, siku moja aliamka nyanya mmoja akamkumbuka nabii Yule. Ndipo aliwaita wazee wa kijijini akawatuma kwake nabi kuomba ushauri. Walipofika walipatiwa kopo la uji wa mtama. Baadaye walisema tatizo lao.Nabii aliwapatia dawa mbili. kwanza akawashauri kubadili tabia zao. kisha akawaambia watubu na kumtolea Mungu sadaka na wote watapona. Walifurahi sana, Watu walipoitumia daa hili, walianza kupona na mifugo yao haikufa tena wala wao wenyewe.

31. Tatizo lipi iliwapata watu wa sehemu ile
A. mifugo ya kufa
B. ugonjwa wa ajabu
C. ongezeko la watu
D. kiangazi
32. Matibabu yalitafutwa kw nani?
A. Waganga
B. Wazee wa kijiji
C. Wachawi
D. Miti shamba
33. Madaktari waliishi wapi?
A. Nchi za mbali
B. Msituni
C. Hapo kijijini
D. Karibu na waganga
34. Ugonjwa huu ulisababishwa na nini?
A. Mazao mengi
B. Tabia za kufuatana
C. Dhambi nyingi
D. Watu kuwa watiifu
35. Watoto hasaa walijulikana kuvunja sharia ipi?
A. Kuwatusi wakuu
B. Kuwaua wazee
C. Kufanya kazi kwa bidii
D. Kuwapiga wenzao
36. Ni kweli kusema
A. vijana walienda shuleni
B. wazee walikuwa wema
C. hawakukuwa na shule
D. vijana hawakwenda shuleni
37. “Kula chumvi nyingi ni
A. kufanya tabia mbaya
B. kula chakula chenye chumvi
C. kujiendeleza kimaisha
D. kuzeeka sana
38. Watu wakubwa walifanya jambo gani ovyo?
A. Kupigana
B. Kulewa
C. Kuwa wazembe sana
D. Kuwaoa wasichana wachanga
39. Wazee walipofika kwa nabii walipewa nini kwanza?
A. Chakula
B. Mkate
C. Uji
D. Chai
40. Dawa walizopewa zilikuwa
A. Kuwahimiza watu kutubu dhambi
B. kula nyama ya kondoo
C. kuwachapa watoto
D. kuenda kwa waganga


Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 41-50
Chui na kifaru walipendana sana.Walikuwa marafiki wa kufa kuzikana kulingana na mapato yao.Kifaru alimpenda chui hata akawa anamwelezea siri zake zote bila kumficha au lolote.Kifaru alipenda sana kwenda huku na kule kutafuta chakula.Chui naye hakupendelea kutoka nyumbani.Wakati ule kifaru alikuwa na pembe mbili zenye makali sana kichwani.Chui alikuwa hana watoto kamwe lakini kifaru alikuwa na watoto wawili.Siku moja kifaru alitoka kwenda kutafuta chakula kama kawaida.Aliwaacha wanawe na chui nyumbani.Kumbe!Chui alikuwa na mipango mibaya.
Baada ya kiamsha kinywa,chui alijifanya kuumwa sana na kuwaomba watoto wa kifaru kupanda mgongoni mwake wamkanyagekanyage.Baada ya muda ,chui alimnasa mtoto mmoja na kumrama bila huruma na kumla.Mtoto wa pili alikimbia na kujificha.Mama kifaru aliporudi nyumbani alipigwa butwaa.Nyumba ilikuwa kimya.Hakukuwa na dalili ya uhai.Alipogunduwa mtoto wake ameuawa na chui,alikasirika sana.Basi vita vikaanza kifaru akamfukuza chui,chui aliruka juu ya mti uliokuwa karibu.Maskini kifaru alijaribu kumshambulia kwa pembe na hapo pembe moja ikakwama na kuvunjika.Leo hii chui hukaa juu ya mti na kifaru amebaki na pembe moja.Pembe hiyo huitwa kipusa.

41. Chui na kifaru walikuwa
A. wakifa
B. wanachukiana
C. wanapendana
D. wakizikana
42. Ni mnyama yupi alitoa siri zake zote?
A. samba
B. kifaru
C. chui
D. kiboko
43. Mnyama aliyependa kutafuta chakula alikuwa
A. kifaru
B. watoto
C. chui
D. chui na kifaru
44. Zamani kifaru alikuwa na pembe
A. nne
B. moja
C. tatu
D. mbili
45. Aliyepanga mabaya ni___________
A. kisui
B. kipusa
C. chui
D. kifaru
46. Kiamsha kinywa ni chakula cha
A. jioni
B. usiku
C. asubuhi
D. mchana
47. Tunaweza kusema
A. chui alikuwa anaumwa
B. kifaru alimla motto
C. chui hakuwa mgonjwa
D. watoto walijificha kichakani
48. Kifaru alipofika nyumbani
A. alishtuka
B. alitoroka
C. alijificha
D. alifukuzwa
49. Pembe fupi wa kifaru iliyo kichwani huitwa
A. pembe
B. jino
C. mkonga
D. kipusa
50. Kichwa mwafaka zaidi kwa taarifa hii ni
A. Chui mgonjwa
B. Watoto wa kifaru
C. Kifaru na chui
D. Chui asiye na watoto




 

More Examination Papers