Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Form 4 Kiswahili Paper 3 End of Term 2 Exams 2021

Class: Form 4

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 4 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1288     Downloads: 40

Exam Summary


JINA_________________________ Nambari: ___________
Sahihi: ____________
Tarehe: ___________
102/3
KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MUHULA WA PILI MWAKA 2021



MUDA: SAA 21/2


MAAGIZO:
1. Jibu maswali MANNE Pekee.
2. Swali la kwanza ni la lazima.
3. Maswali mengine yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki.
4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
5. Kila swali lina alama ishirini







1.SEHEMU A: USHAIRI (LAZIMA)
Eti
Mimi niondoke hapa
Niondoke hapa kwangu
Nimesaki, licha ya risasi
Vitisho na mauaji, siondoki

Mimi
Siondoki
Siondoki siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Kwa mateke hata na mikuki
Marungu na bunduki, siondoki

Hapa
Siondoki
Mimi ni Pahame!
Niondoke hapa kwangu!
Fujo na ghasia zikizuka
Na kani ya waporaji, siondoki

Haki
Siondoki
Kwangu siondoki
Niondoke hapa kwangu!
Nawaje; waje wanaokuja
Mabepari wadhalimu, siondoki

Kamwe
Siondoki
Ng’oo hapa kwangu!
Katizame chini mti ule!
Walizikwa babu zangu, siondoki

Sendi
Nende wapi?
Si hapa kitovu changu
Niondoke hapa kwangu
Wangawa na vijikaratasi
Si kwamba hapa si kwangu, siondoki

Katu
Siondoki
Sihitaji karatasi
Niondoke hapa kwangu
Yangu mimi ni ardhi hii
Wala si makaratasi, siondoki


Maswali
1.
a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini (alama 2)

b) Taja masaibu anayopitia mzungumzaji (alama 4)

c) Eleza toni ya shairi hili (alama 2)

d) Eleza muundo wa shairi hili (alama 3)

e) Tambua matumizi ya mbinu ya usambamba (alama 2)

f) Andika ubeti wa tano kwa lugha nathari (alama 4)
g) Tambua idhini moja ya mtunzi (alama 1)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi (alama 3)
(i) Karatasi
(ii) Nimesaki
(iii)kitovu

2.SEHEMU B TAMTHILIA YA KIGOGO
2.Uliona nini kwa huyo zebe wako ? Eti mapenzi!
a. Eleza muktadha wa dondoo. (al. 4)
b. Andika mbinu za lugha zinazojitokeza kwenye dondoo hili (al. 4)
c. Taja hulka za mnenaji unajitokeza katika dondoo. (al. 2)
d. Mwanamke ni kiumbe wa kukandamizwa. Thibitisha kauli hii ukirekjelea tamthilia.
(al. 10)
3.wa kurejelea tamthlia ya 'Kigogo ya Pauline Kea, onyesha jinsi ambavyo viongozi wengi katika nchi za kiafrika wamejawa na tamaa. (alama 20)


SEHEMUC.RIWAYA YA CHOZI LA HERI(ASSUMPTA MATEI)

4.“ Kwa kweli ni hali ngumu hii”
Weka dondoo katika muktadha wake. (alama4)
Ni hali gani ya msemewa inayorejelewa kwenye dondoo. (alama16)

5) Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika. Tetea kauli hii ukilejelea Chozi la Heri ( al. 20)



Alifa Chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi nyingine
jibu swali la 6 au la 7
6.Ukirejelea hadithi zifuatazo, eleza jinsi maudhui ya mapenzi na asasi ya ndoa yanavyojitokeza. (alama20
a) Mapenzi ya kifaurongo
b) Masharti ya kisasa
c) Ndoto ya Mashaka
d) Mtihani wa maisha
Au

Shibe inatumaliza : Salma Omar Hamad
7.“Hiyo ni dharau ndugu yangu. Kwa nini kila siku tunakula sisi kwa niaba ya wengine ?”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
b) Eleza sifa za msemaji. (alama 6)
c) Eleza jinsi viongozi wanavyokuwa wabadhirifu. (alama 10)






SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
8a) Fafanua mchakato/fomula ya uwasilishaji wa vitendawili. (alama4)
b) Linganisha naulinganue vitendawili na methali. (alama10)
c) Toa sababu sita za kudidimia kwa fasihi simulizi. (alama6)

 

More Examination Papers