Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
Form 3 Paper 3 Kiswahili End of Term 2 Exams 2021
Class: Form 3
Subject: Kiswahili
Level: High School
Exam Category: Form 3 End Term 2 Exams
Document Type: Pdf
Views: 1272
Downloads: 20
Exam Summary
MITIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI, MWAKA 2021
KIDATO CHA TATU
KISWAHILI
KARATASI YA 3 (102/3)
FASIHI
JINA ………………………………………..NAMBA YA KUSAJILIWA…………………..
JINA LA SHULE ………………………………………DARASA……………………………
TAREHE…………………………………….
MUDA: Saa 2 ½
MAAGIZO KWA WATAHILIWA
a) Jibu maswali manne pekee.
b) Swali la kwanza ni la LAZIMA.
c) Chagua maswali mengine matatu kutoka sehemu nne zilizobaki yaani; Ushairi, Riwaya,Hadithi fupi na Tamthilia.
d) Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
e) Kila swali lina alama 20
f) Majibu yote yaandike kwa lugha ya Kiswahili.
Karatasi hii ina kurasa 4 zilizochapishwa. Wagombea wanapaswa kuangalia ilikuhakikisha kuwa kurasa zote zimechapishwa kama ilivyoonyeshwa na kwamba hakuna maswali yanayo kosekana.
SEHEMU YA A: FASIHI SIMULIZI
1.
a) Taja mifano minane ya vipera vya utanzu wa semi katika fasihi simulizi. (alama4)
b) Fafanua sifa zozote tatu za mawaidha katika fasihi simulizi (alama3)
c) Eleza umuhimu tatu wa ngomezi. (alama3)
d) Eleza istilahi hizi za fasihi simulizi. (alama3
i) Maghani
ii) Mapisi
iii) Misimu/simo
e) Fafanua sifa zozote tatu ambazo mtambaji wa hadithi anastahili kuwa nazo. (alama3)
f) Taja methali zozote mbili zilizo na dhana ya tashibihi. (alama2)
g) Eleza sifa zozote mbili za nyimbo. (alama2)
SEHEMU YA B: USHAIRI
2. Soma shairi lifuatalo kasha ujibu maswali yanayofuata
Mkata ni mkatika,harithi hatoridhiwa
Sina ninalolishika,wala ninalochukuwa
Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!
Mrithi nini wanangu?
Sina ngo’mbesi na mbuzi,sina konde sina buwa
Sina hata makaazi,mupasayo kuyajuwa
Sina mazuri makuzi,jinsi nilivyoachwa
Mrithi nini wanangu?
Sina kazi sina bazii la wingi wa shakawa
Sina chembe ya majazi mnoni kukamuliwa
Nakwa’cheni upagazi,ngumu kwenu ku’tuwa
Mrithi nini wanangu?
Sina sikuachi jina,mkata hatasifiwa
Hata nifanye la maana,mnoni kulaumiwa
Poleni wanangu sana,sina kwenu cha kutowa
Mrithi nini wanangu?
Sina leo sina jana,sina kesho kutwaliwa
Sina zizi sina shina,wala tawi kuchipuwa
Sina wanangu mi,sina,sana la kuacha kuraduwa
Mrithi nini wanangu?
Sina utu sina haki,mila yangu meuliwa
Nyuma yangu ilidhiki,na mbele imekaliwa
N’nawana namiliki,hadi nitakapofukiwa
Mrithi nini wanangu?
Sina ila kesho kwenu,wenyewe kulongowa
Muwane kwa nyinyi mbinu,mwende pasi kupumuwa
Leo siyo kesho yenu,kama mutajikamuwa
Mrithi nini wananngu?
MASWALI
a) Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha wanawe. (alama2)
b) Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe. (alama3)
c) Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama4)
d) Dondoa mifano miwili miwili ya: (alama2)
i. Inkisari
ii. Tabdila
i. Chambua shairi hili kwa upande wa: Dhamira (alama2)
ii. Muundo (alama4)
e) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika shairi. (alama3)
i. Mlimwengu kanipoka
ii. Sina konde sina buwa.
iii. Wingi wa shakawa.
SEHEMU YA C: RIWAYA
A.K Matei: Chozi la Heri
3. Malezi ya watoto katika riwaya ya Chozi la Heri ndicho kitovu cha ufanisi na matatizo yote yanayowapiku watoto. Jadili (alama 20)
4. “…, Di, ni mimi… niko hai. Auntie Sauna alishikwa na polisi. ’’
a) Liweke dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
b) Fafanua sifa za msemaji. (alama 6)
c) Eleza tamathali moja ya lugha iliyotumika katika dondoo hii. (alama2)
d) Sauna alishikwa na polisi? Elezea kikamilifu (alama 8)
SEHEMU YA: D HADITHI FUPI
A.Chokochona D.Kayanda:
Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyinginezo
5. "Penzi lenu na nani? . . . . Mgomba changaraweni haupandwi ukamea. Potelea mbali mkate wee!"
a) Eleza muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
b) Taja na ufafanue mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. (alama 4)
c) Onyesha vile maudhui ya utabaka yanavyojitokeza katika hadithi nzima. (alama 6)
d) Eleza sifa sita za mzugumzaji kwenye dondoo. (alama 6)
6. Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika riwaya ya, ‘Tumbolisiloshiba na hadithi nyingine.’ Jadili maudhui ya nafasi yawazazikatikamalezi. (alama 20
SEHEMU YA E: TAMTHILIA
P.Kea: Kigogo
7. Tamthiliaya “Kigogo” ni kioo cha uhalisia wa maisha ya jamii nyingi za Kiafrika. Thibitisha. (alama 20
More Examination Papers