Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Grade 1 Kiswahili Activities End of Term 2 Examination 2021

Class: Grade 4

Subject: Kiswahili Activities

Level: Primary School

Exam Category: Grade 4 End Term 2 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1372     Downloads: 18

Exam Summary


COMPETENCY BASED CURRICULUM
GRADE 4 TERM 2 2021
KISWAHILI SECT. B ACTIVITIES ASSESSMENT
SEHEMU YA III: MATUMIZI YA LUGHA

Tambua vitanzandimi katika sentensi zifuatazo (Ala 4)
1. Baba alivua papa katika bahari pana.

2. Kila chacha akila hali chakula kikichacha

3. Jana mama alichana nywele mapema.

4. Kuku anachakura chakula mchangani.

5. Nomino ni nini? (Ala 2)

Tumia Nomino zifuatazo katika kuunda sentensi (Ala 3)
(Magonjwa, viwanda, kiti)
6.______________________________________________
7.______________________________________________
8.______________________________________________

9. Je ni maneno gani huwa tunatumia kurejelea sifa ya kitu? k.m safi huitwaje? (Al 1)

Jaza nafasi zilizoachwa kwa kutumia vivumishi sahihi kwenye mabano. (Al 4)
10. Huyu ni rafiki _____________ (yangu, zetu)

11. Hizi ni meza__________ (zetu, changu)

12. Hiki ni kitabu _________ (vyangu,changu)

Weka mstari chini ya kiwakilishi. (Al 3)
13. Yeye ni mwanafunzi katika shule yetu.

14. Mimi ni mwanafunzi bora katika darasa letu.

15. Mzazi yule anapendeza sana.

16. Eleza maana ya kitenzi na kutoa mfano. (Al 2)

17. Piga mstari chini ya vitenzi katika sentensi zifuatazo (Al 5)
a. Mwalimu anacheza kandanda kiwanjani.

b. Mpishi amepika chakula kitamu sana.

c. Gari letu linaendeshwa mbio sana.

d. Kuku anachakura chakula topeni.

e. Tunafaa kusoma kwa bidii ili kufaulu katika mtihani.

Taja salamu zinazotumika katika nyakati zifuatazo (Ala 4)
18. Wakati wa jioni

19. Wakati wa asubuhi

20. Nyakati za usiku

21. Wakati wa mchana

SEHEMU YA IV: UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Ufisadi imekuwa jangaa kubwa katika nchi yetu ya Kenya. Katika miji mikubwa, madogo na vijijini ufisadi imekuwa jambo la kawaida. Watu hushiriki ufisadi kwa njia mbalimbali kama vile kupata huduma mbalimbali, kupata kazi, kuepuka kupelekwa korokoroni na vilevile kusafirisha bidhaa bandia kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Nchi ya Kenya inapoteza takribani bilioni 20 kila mwaka katika ufisadi. Kwa sababu hii huduma zinazofaa kuwafikia wananchi haziwezi kama vile: barabara kujengwa, elimu bora, kujenga hospitali na kupata maji safi. Hivi karibuni tumeshuhudia pesa zinazofaa kuwa za kuwasaidia wananchi katika vita dhidi ya korona zikinyakuliwa hadharani kana kwamba vyongozi hawana utu huku wagonjwa wa Korona wakifa kila uchao.
Hili ni jambo ambalo kwa sasa limetufikia ukingoni na hatuwezi nyamaza kamwe. Ni lazima tusimame imara kupiga vita dhidi ya ufisadi.Hili ni jukumu langu na lako. Hatuwezi kuruhusu jamii ya kesho kuangamia kwa sababu ya makosa tunayofanya sasa. Mikakati mbalimbali yafaa kuwekwa ili kuepuka jangaa hili kuhudhuru jamii yetu kama vile, kuweka hukumu ya Maisha kwa wale wanaopatika katika ufisadi, kufudisha wananchi kuhusu maadili, kurejesha masomo kuhusu maadili shuleni na iwe kama kozi maalum na pia kuwaelimisha wananchi kuhusu ufisadi.
22. Ni njia zipi tunazoweza kutumia kuzuia ufisadi (Al 3)

23. Eleza njia tatu ambazo ufisadi hutokea (Al 3)

SEHEMU YA V: KUANDIKA
Wewe ni Mkenya halisi anayejua viongozi wake. Andika insha ya Wasifu kuhusu kiongozi yeyote unayempeda.

 

More Examination Papers