Kiswahili Paper 3 Form 4 End of Term 1 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions
SEHEMU YA A: USHAIRI
1.LAZIMA
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yatakayofuata
Sikatai, kujirembesheni, bali kuzidisha,
Sikatai, kujikwatueni, bali kupitisha,
Sikatai, kujitw
ezeneni, ila kujishusha,
Sikatai, kuzidisheneni, bali kupimeni.
Sikatai, kwenda uzunguni, ila kuzidisha,
Sikatai, kuweka herini, bali si kutisha,
Sikatai, rangi midomoni, ila ‘ogopesha,
Sikatai kuzidisheneni, bali kupimeni.
Sikatai, kuharamisheni, ila kupitisha,
Sikatai, kurandarandeni, sio ‘korofisha,
Sikatai, kuzungumuzeni, wala kuchekesha,
Sikatai, kuzidisheneni, bali kupimeni.
Sikatai, kuharamisheni, hata halalisha,
Sikatai, kuchungachungeni, sio ‘haramisha,
Sikatai, usiogopeni, ila rekebisha,
Sikatai, kuzidisheneni, bali kupimeni.
Sikatai, kuwa limbukeni, bali elimisha,
Sikatai, kuwa hayawani, bali rekebisha,
Sikatai, kuwa punguani, ila aibisha,
Sikatai, kuzidisheneni, bali kupimeni,
Sikatai, kuomba ombeni, ila kunashusha,
Sikatai, kuwa masikini, ila fedhehesha,
Sikatai, kuendeleeni, bali tamatisha,
Sikatai, kuzidisheneni, bali kupimeni.
MASWALI
(a) Lipe shairi ulilolisoma anwani mwafaka. (alama 1)
(b) Eleza dhamira ya mshairi wa shairi hili. (alama 1)
(c) Weka shairi hili katika bahari tofauti na utoe sababu. (alama 3)