Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
Kiswahili Paper 2 Form 4 End of Term 1 Examination 2019
Class: Form 4
Subject: Kiswahili
Level: High School
Exam Category: Form 4 End Term 1 Exams
Document Type: Pdf
Views: 1170
Downloads: 21
Exam Summary
Kiswahili Paper 2 Form 4 End of Term 1 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions
UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Ni dhahiri shairi kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za karibuni.Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda ya Afrika mashariki.Taarifa za Uharamia zimetawala vyombo vya habari. Kiasa cha kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia na nchi husika, simanzi na masaibu yasiyoweza kutiwa kwenye mizani.
Yamkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwana kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa. Aghalabu, suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mijini Nairobi na Dar es Salaam mnamo Agosti 7.1998 na tukio la septemba 11, mwaka 2001 kule marekani. Maafa na uharibifu wa mali si hoja, la maana kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao.Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala wajibika katika maeneo kunakotokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingira yanayowezesha na kuruhusu kuchipuka kwa janga hili.
Mchipuko wa baa la uharamia umelenga jamii ya kimataifa ambayo ni mhudumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliyoshesheni pakubwa barani.Bila shaka, hili ni suala linalilozalishwa kinyume mbele. Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulimwenguni.
Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo matumizi ya nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa,kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni. Aidha, utawala wa nchi kunakochipuka uharamia haujajizatiti kuharamisha doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa, inayochangia upungufu na ucheleweshi wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi.Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwenguni. Ni muhali kwa utalii kustawi kwenye maeneo yaliyo na tishio la usalama, ikakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
Jitahidi za kuweka laini mawasiliano chini ya bahari ili kurahisisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kutafutia juhudi za maharamia katika bahari Hindi. Kwa mujibu wa hali hii, mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni.Licha ya hayo, shughuli za uvuvi na biashara nyenginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba. Itabidi mikakati na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze kusitishwa.
Maswali
a) Kwa nini uharamia umetamalaki ulimwenguni? (alama 3)
b) Uharamia unaelekea kumtia hofu mwandishi.fafanua. (alama 3)
c) Thibitisha kwa kuwa Kenya imeathirika pakubwa kutokana na vitendo vya uharamia. (alama 4)
d) Fafanua dhana ya “kinyume-mbele” kwa mujibu wa taarifa hii. (alama 2)
e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya
(alama 3)
i) Uharamia
ii) Mtandao
iii) Mwambao
More Examination Papers