Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Paper 2 Form 4 End of Term 1 Examination 2020

Class: Form 4

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 4 End Term 1 Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1506     Downloads: 41

Exam Summary


Kiswahili Paper 2 Form 4 End of Term 1 Examination 2020
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


1. UFAHAMU (Alama 15)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Nimekaa na kutafakari kwa kipindi kirefu, juu ya mabilioni ya pesa ambayo yametengwa na serikali ili kudhamini miradi ya maendeleo ya wanawake. Kina mama au wanawake wengi wanakiri na kusema kwamba fedha hizo zimewezesha kuwaondoa katika lindi la unyanyasaji kutoka kwa waume zao.Kwani kila mmoja anamheshimu mwenzake kwa sababu ya kipato alicho nacho. Wengi wameweza kuanza biashara ndogondogo ambazo huwaletea angaa kipato kidogo.
Ukweli ni kwamba fedha hizi zimesaidia kuwatoa wanawake wengi katika unyanyasaji,kwani wengi wanaweza kuanzisha kazi za ujasiriamali na hata kuendesha shughuli mbaimbali za maendeleo.
Kutokana na mafanikio haya, wabunge waliopitisha hoja bungeni za kuanzisha mpango huu wa kuwakwamua wanawake kimaendeleo wanafaa kupongezwa. Mafanikio haya yamewafanya akina mama kujikimu kimaisha na hivyo kutowategemea wanaume katika kila jambo.
Ukitaka kujua ukweli kuhusu hili, nenda kwenye masoko utaona akina mama jinsi wanavyohangaika na biashara zao. Kwa hivyo, ujasiriamali huendelezwa na akina mama zaidi na hivyo wanapaswa kuwezeshwa kwa hali na mali.
Akina mama pia wanafaa kupongezwa kwani wameamua kujitosa kukopa fedha kutoka kwenye taasisi mbalimbali za fedha. Fedha hizo kwa kiwango kikubwa zimewainua kutoka katika ufukara uliokithiri hadi katika maisha ya heshima.Wale ambao hawajajaribu kuchukua mikopo, ni muhimu wafanye hivyo ili wajikimu kimaisha.
Maisha ya sasa ni magumu, hivyo yanahitaji kusaidiana kwa kila hali na mali.Wanaume kwa wanawake ni vyema wachange bia ili wazumbue riziki.Ushirikiano utarahisisha maisha yao. Hata hivyo, sio tu akina mama hao wameondokewa na unyanyasaji waliokuwa wakiupata ndani ya nyumba zao, toka kwa akina baba, bali hata masualama ya mrundikano wa kesi za kugombea ardhi kwa akina mama, zimepungua. Sababu ni kwamba akina mama wengi wameweza kujitafutia ardhi wenyewe kwa fedha walizonazo.
Ukweli ni kwamba hali imebadilika. kinyume na hapo awali, ambapo majumba ya kifahari na mashangingi yalikuwa hifadhi ya wanaume, siku hizi wanawake wanamiliki hayo yote.

 

More Examination Papers