Kiswahili Paper 3 Form 3 End of Term 1 Examination 2020
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions
SEHEMU A;USHAIRI
1.Lisome shairi hili kasha ujibu maswali
Msituni nikakuta ,Nyuki wamo mzingani,
kwa juhudi wanakita ,mara nje mara ndani,
Husuda wameikata,hata hawasengenyani,
Nyuki ni wadudu duni,wanashinda kwa umoja.
Mchwa nao nikaona ,wamejenga masikani,
Wafanya bidii sana,uvivu hawatamani.
Wao husaidiana ,tena hawadanganyani
Mchwa wadudu wa chini,wanaishi kwa umoja.
Nalo jeshi la siafu,hutandawaa njiani,
Laenda bila ya hofu,maana lajiamini,
Silaha zao dhaifu,meno,tena hawaoni,
Wa kuwatadia nini?kwani wanao umoja
Nao chungu wachukuzi,nyama warima njiani,
Masikini wapagazi,mizigo ya kichwani,
Ingawa si wachokozi,wakali ukiwahini,
Katu hawafarakani,wanadumu kwa umoja.
Sisi ni wana Adami,mbona hatusikizani,
Tusiletie hamu,ukubwa kuutamani,
Wachache wataalamu,tuwasidi kwa imani
Hii “huyu awezani” Yatuvunja umoja