Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
Kiswahili Form 1 End of Term 1 Examination 2020
Class: Form 1
Subject: Kiswahili
Level: High School
Exam Category: Form 1 End Term 1 Exams
Document Type: Pdf
Views: 3492
Downloads: 121
Exam Summary
Kiswahili Form 1 End of Term 1 Examination 2020
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions
Jibu maswali yote kwenye nafasi zilizoachwa wazi.
Mawasiliano ni neno ambalo asili yake ni wasili. Wasili lina maana ya kufika kwa mtu, kitu, au jambo fulani baada ya mwendo au safari. Kwa hivyo kuwasiliana kuna maana watu, kitu au mambo kufikiana kutoka mahali.
Katika siku za jadi mawasiliano yalikuwepo lakini ya shida. Hata hivyo, watu waliwasiliana kwa kutumia moshi, ngomezi au kupiga mbiu. Mbinu hizi za jadi zilitumiwa baina ya vijiji ili kujulisha wanakijiji jambo la dharura au kuwajulisha jambo lingine lolote. Mbiu ilitumika kwa jambo la dharura. Njia za kusafirisha mizigo zilikuwa haba. Baadhi ya watu walitumia wanyama, kama fahali au farasi kukokotea mizigo yao.
Siku hizi mawasiliano yamepanuka sana. Mawasiliano ya kisasa yanahusisha simu, mtandao, televisheni na wavuti. Mawasiliano ya kisasa yamefanya ulimwengu wa kisasa kuwa kijiji kimoja kikubwa.
Kwa kuzingatia maudhui haya, vyombo au njia kama redio, simu, waraka, ndege, meli, motokaa na wavuti vimepewa jina la vyombo vya mawasiliano. Hivyo basi yafaa tutathmini ni vipi vyombo au njia hizi hufanya kazi ya kuwasiliana na huwasilisha nini. Vyombo hivi vinaweza kuelezwa chini ya vichwa vitatu; usafiri, mazungumzo na picha. Vyombo mathalan baiskeli, ndege, meli na magari hufanya kazi ya kuwasafirisha watu kutoka janibu moja hadi nyingine. Watu wanaposafiri huwa wanasafirisha mali yao. Bidhaa kama kahawa, vyuma na mizigo mingine husafirishwa kwa meli, ndege na magari kupitia majini, hewani au barabarani.
Bandari, viwanja vya ndege na barabara zimeimarishwa ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo. Anayesafirisha bidhaa fulani na wakati huo anatakikana kukusanya nyingine, inamlazimisha asiambatane na bidhaa hizo lakini ahakikishe zimewasili alikozikusudia. Hivyo basi njia nyingine ya mawasiliano ilivumbuliwa.
Njia hii ambayo ni mazungumzo hutumia vifaa kama barua, simu, barua pepe na kipepesi. Mtumiaji ataandika ujumbe na kuutuma kupitia shirika la posta au mashirika mengine ama mtandao. Yamkini ilihitajika kuweza kujibizana na kuulizana kati ya watu hao wawili ndipo simu ilipovumbuliwa na kumwezesha mtu kuzungumza na mwingine akiwa mbali sana. Watu huzungumza na kufahamiana. Ilipohitaji mtu kukiona kitu anachozungumzia ndipo ilibidi kuunda vifaa vya kuonyesha picha kama vile televisheni.
Ilikuwa fahari kubwa sana kwa Wakenya kuwasiliana na nchi ya Ghana wakati wa michuano ya mpira ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika. Wakenya waliweza kuiona michezo hiyo moja kwa moja ingawa kijiografia Kenya na nchi hiyo zina majira tofauti.
More Examination Papers