Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 3 Opener Term 1 Examination 2020

Class: Form 3

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 3 Opener Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1422     Downloads: 19

Exam Summary


Kiswahili Form 3 Opener Term 1 Examination 2020
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


SEHEMU YA A:UFAHAMU: ALAMA 15
Vitabu vingi vya hadithi za watoto vilivyowahi kuandikwa katika lugha ya Kiswahili kufikia sasa vinaweza tu kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa darasa la nne hadi la nane na hivyo basi, kuacha ombwe pale panapostahili kuwekwa msingi imara – shule ya chekechea hadi darasa la tatu. Utafiti uliowahi kufanywa na wanaisimu- saikolojia unathibitisha kwamba, uwezo wa mwanafunzi wa kujifunza lugha ya pili huwa katika kiwango cha juu awapo na umri mdogo na kwamba, uwezo huo huanza kupungua kadiri umri unavyoongezeka na kufikia kipindi maalum (critical period) ambacho hukisiwa kubisha katika umri wa kubaleghe au kuvunja ungo.
Hivyo basi, ili kustawisha hulka ya usomaji ya kudumu, waandishi wa fasihi ya watoto wanapaswa kujifahamisha mengi kuhusu ukuaji wa watoto hao wadogo na mikakati ambayo huitumia katika kujifunza lugha ya pili.
Aidha, wanapaswa kuyafahamu yale yanawapendeza na kuwachochea katika kusoma ili kuyajumuisha katika vitabu vyao vya hadithi. Mambo haya yatatimia iwapo waandishi hao watakuwa na mafunzo ya kimsingi katika taaluma ya isimusaikolojia.
Wanafunzi katika viwango tofauti wana mikakati tofauti ya kujifunza lugha ya Kiswahili. Kufikiria kwamba wanafunzi wa madarasa ya chini (darasa la kwanza, pili na tatu), wanaweza kuitumia mikakati sawa na ile ambayo hutumiwa na wenzao wa madarasa ya juu kujifunza Kiswahili si sahihi.
Watoto wadogo hujifunza mambo mengi kwa kukariri, kuigiza, kuiga, kufuatilia hadithi kwa picha miongoni mwa mbinu nyingine. Ili kufanikiwa katika kuwaandikia, sharti mikakati hiyo ya ujifunzaji izingatiwe.
Ufundi mkubwa unahitajika sio tu katika kuziunda sentensi zao, bali pia katika kuifinyanga sarufi. Sentensi zenyewe ziwe fupi, zenye sarufi na msamiati sahihi, zilizorudiwarudiwa ili kuzifanya zinate akilini na kuendelezwa kwa mtindo wa nyombo au mashairi mepesi.
Watoto wadogo huvutiwa sana na nyimbo na mashairi mepesi na hujifunza kwa urahisi kupitia kwayo. Msururu wa vitabu vya 'Someni kwa Furaha' uliotumiwa katika miaka ya themanini na mwanzomwanzo wa miaka ya tisini, ni mfano wa vitabu vilivyotekeleza dhima muhimu sana katika kuumua na kuchochea hamu ya wanafunzi kupenda kukisoma Kiswahili.
Vitabu vilitumia mbinu mbalimbali zilizoweza kuyateka mawazo ya wanafunzi katika viwango tofauti. Miongoni mwa mbinu hizo ni matumizi ya vibonzo, mashairi na nyimbo za chekechea zenye maudhui ambayo watoto wangeweza kujinasibisha nayo. Baadhi ya nyimbo hizo zilihimiza umuhimu wa kusomea katika mazingira safi, ushirikiano katika shughuli mbalimbali na umuhimu wa kuyachangamkia masomo. Mfano mzuri ni huu wimbo unaopatikana katika kimojawapo cha vitabu katika msururu huo: chawa chawa mchafu, petu ni pakavu. Kata nyika utosini, kata nywele kwa mashine. Kichwa safi kama nini? Chawa chawa mchafu petu ni pakavu.

 

More Examination Papers