Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.

Kiswahili Form 2 Opener Term 1 Examination 2020

Class: Form 2

Subject: Kiswahili

Level: High School

Exam Category: Form 2 Opener Exams

Document Type: Pdf

    

Views: 1797     Downloads: 53

Exam Summary


Kiswahili Form 2 Opener Term 1 Examination 2020
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions


A. UFAHAMU (ALAMA 15)
Yasemekana kuwa Shungwaya ndicho kitovu cha watu waishio Giriama katika janibu za pwani ya Kenya na wanaojulikana kwa jumla kana Wamijikenda. Yaaminika kuwa bado wakiwa Shugwaya, walimuua Mgalla mmoja mwenyeji wa Shungwaya na kitendo hicho kiliamsha hasira kali za Wagalla, hata ikawawia vigumu Wamijikenda kuishi kwa usalama pamoja na ndugu zao hao.
Hata hivyo, Wamijikenda hawakugura mara moja wala wote kwa pamoja bali walihama katika vipindi tofuati na katika makundi madogomadogo. Kila kundi lililofika Giriama lilijenga ‘kaya’ au mji wake. Kwa jumla, walihama kwa makundi tisa.
Vile vile, Wamijikenda walihama na fingo yao ambayo ilifukiwa na viongozi wao katikati ya kaya zao, palipokuwa na msitu mdogo. Hakuna ajuaye hasa mahali ilipofukiwa ila wazee hao waliopenda kufanyia baraza mahali hapo.
Mnamo mwaka wa 1870, mzee Menza na mkewe walibarikiwa kufungua kizazi kwa kupata mtoto wa kike waliyemwita Mekatilili. Walimlea vizuri na alipoanza kuzungumza, alionyesha dalili za kuwa na kipawa cha pekee. Kwanza, alipenda kujua kila kitu kilichoihusu jamii yake na pili alichukizwa sana na kiumbe aliyemdhulumu kiumbe mwenzake. Kwa mfano, aliwaonea vipepeo imani walipoliwa na ndege. Tena alizipenda sana mila na desturi za watu wa jamii yake – Wamijikenda.
Siku moja, baada ya Mekatilili kufikia utu uzima, mama yake alimwita chemba akamwambia, “Mwanangu sasa umeshabalehe, nami ningependa kuwaona wajukuu wangu kabla sijawafuata wazee waliotangulia. Waonaje tukikuoza? Mimi na baba yako tumepata mume ambaye ni kufu yako kabisa.”
“Ninaelewa, maana hizi ni desturi zetu, lakini ningefurahi zaidi kama mngeniruhusu nijichagulie mume ninayempenda.” Binti alimjibu mamaye.
“Mnazi na uwe mrefu, huyumba kufuata upepo.” Mama akajibu. Tangu hapo binti akawa hana la kujibu ila kukubali.
Siku ya harusi, watu wengi walihudhuria na wakastarehe kwa tembo la mnazi ambalo lilikuwa limetengenezewa kwa wingi. Jioni hiyo, mekatilili alichukuliwa kwa mumewe Masendeni, karibu na mto Sabaki. Ikawa hangeonana na wazazi wake kila siku kama ingalivyokuwa mapenzi yake. Wakati huu kote nchini Kenya kulikuwa kumejaa wageni, wengi wao wakiwa walowezi na watawala wa kibeberu. Walikuwa wameanzisha mashamba ya mikonge, kahawa na chai. Walihitaji watu wa kupalilia mashamba yao hayo. Hata hivyo Waafrika hawakuwa na haja ya kulima wala pesa. Hata walipolima, ni kwa minajili ya kubadilishana mazao na kula.Iliwabidi Wazungu kutumia mizungu ili kuwashurutisha Waafrika kuwalimia. Baadhi ya mikakati waliyobuni ni kuwateka nyara watu barobaro na kutoza kodi. Ni katika harakati kama hizo ambapo mumewe Mekatilili alitekwa, asirudi tena kwake. Wakati uo huo, wazazi wa Mekatilili waliaga dunia.
Mambo haya yalimpa mekatilili msukumo. Baada ya muda wa kuomboleza kuisha, alijiunga na wazee wapigania ukombozi, mmoja wao akiwa Wanje, kakaye mumewe. Aliwaunganisha wanawake na kuwahimiza wasiige mila na desturi za kizungu. Aliwahutubia wanaume na kuwakumbusha kuwa ilikuwa lazima wailinde nchi yao. Siku moja alishikwa kwa kuwalisha watu kiapo. Alipelekwa bara, Kisii, mbali kabisa na kwao, Masharibi mwa Kenya na akatiwa kizuizini pamoja na Wanje. Hata hivyo, walifaulu kutoroka na kwa muda wa siku ayami walipitia kwenye mabonde na milima, misitu na nyika hadi wakarudi Giriama.
Mabeberu walikasirika sana. Hata hivyo, walikuwa wamechelewa. Katika safari yao kurudi Giriama, walifaulu kuhubiria wengi dhidi ya mgeni. Vita vya ukombozi vilikuwa vimeshika.

 

More Examination Papers