Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
Kiswahili Form 2 End of Term 3 Examination 2019
Class: Form 2
Subject: Kiswahili
Level: High School
Exam Category: Form 2 End Term 3 Exams
Document Type: Pdf
Views: 1535
Downloads: 41
Exam Summary
Kiswahili Form 2 End of Term 3 Examination 2019
This file contains questions and the Marking scheme in it. Below is a preview of the questions
UFAHAMU(ALAMA 15)
Dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. Ni zimwi linalotesa na kufisha wazee kwa vijana. Halichagui jinsia, tabaka, rangi wala umri. Uraibu wa dawa hizi hauna faida yoyote. Wanaotumia dawa za kulevya huzitia mwili kwa kunusa, kuvuta, kumeza na kujidunga sindano. Zinapoingia katika miili ya watu madhara huwa mengi.
Kuna wale wanaokosa hamu ya kula, wengine huambukizwa maradhi kama vile ukimwi wanapotumia sindano zilizotumiwa na watu wenye virusi vya maradhi hayo kujidunga sindano na kutia dawa mwilini.
Mihadarati pia inaweza kufanya mtu awe mwendawazimu. Vifo pia hutokea ikiwa uraibu utazidi na mtu akose kupata matibabu. Mtu anayetumia dawa za kulevya huathirika akili. Yeye huwa hana uamuzi wenye hekima katika maisha yake .wengi wao hushiriki katika vitendo vya uhayawani. Wao hukosa fikra za utu. Baadhi yao wamebaka kina mama na watoto wadogo na wengine wamezua vita katika familia na kusababisha madhara makubwa katika jamii zao kwa sababu ya ulevi.
Familia za wanaotumia mihadarati hazina amani. Jamaa zao hutumia hala nyingi kuwalipia ada ya hospitali ili wapate matibabu baada ya kuzidiwa na uraibu. Mali hufujwa na watu wenye uraibu wa dawa hizo pale wanapohakikisha hawazikosi kila siku. Mzazi kwa mfano anaweza kutumia hela kununua dawa za kulevya badala ya kumlipia mwanawe karo. Kuna wale wanaowaibia majirani na marafiki ili wakidhi mahitaji yao.
Ajali barabarani pia husababishwa na malevi. Dereva yeyote awe wa matatu au gari la kibinafsi anapoedesha gari akiwa mlevi huwa anahatarisha maisha yake mwenyewe, abiria na wananchi wanaopiga miguu barabarani .Uchumi wa taifa huzorota baada ya wananchi kutumia mihadarati. Watu wenye uraibu hukaa mbumbumbu bila kufanya lolote hasa kutokana na kudhoofika kwa afya yao au ulegevu unaosababishwa na ulevi. Watu wa aina hiyo huwa wanamchango haba katika ukuzi wa uchumi wa taifa.
Dawa hizi zimesambaa kila mahali utapata zinauzwa masokoni, shuleni, njiani na hata pahali popote pale penye watu. Dawa za kulevya haziuzwi hadharani nchini Kenya kwa sababu serikali imepiga marufuku uuzaji wa bidhaa hiyo. Waja wanaoziuza hufanya hivyo kisiri. Walanguzi wa mihadarati aghalabu hutumia watu wengine kuuza kwa niaba yao. Kuna wale wanaotumia watoto , wanaorandaranda almaarufu chokoraa na wengine hutumia vijana katika shule za misingi, upili na vyuo vikuu kama mawakala.
Vijana hasa wamejipata katika mtego huu kwa kuwafanyia walanguzi biashara hii haramu hili waweze kupata hela za kukidhi matakwa yao ukweli ni kuwa pesa wanazo patiwa na waajiri wao ni chache mno na hatimaye wao hutumia daw zile na kuishia kuwa na uraibu unaosababisha wao wenyewe kuwa wateja wa mabwenyenye hao wasio na utu.
Watu maarufu kama vile wafanyabiashara, wanamuziki na wanasiasa wametuhumiwa kushiriki katika biashara hii . washukiwa hawa mara nyingi hukosa kufikishwa mahakamani kwa sababu jamii hukosa ushahidi wa kutosha dhidi ya tabia hiyo. Ni nani hasa muhusika katika kuingiza sumu hii katika nchi yetu ? hakuna mtu anayeweza kusimama kadamnasi na kusema hiyo ndiyo kazi yake. Mbona tushiriki katika biashara tusiyoweza kujivunia?
Ni mwito wangu kwa kila mwananchi mzalendo kuungana na wenzake ili kupinga biashara hii haramu. Tuhubiri makanisani, shuleni misikitini, hekaluni na mahali popote pale. Tukemee adui huyu, wa afya na mali. Washauri nasaha washike usukani wawashauri wazee kwa vijana, wakubwa kwa wadogo, weusi kwa weupe tuizike mihadarati katika kaburi la sahau.
Maswali (al.15)
1. Yape makala haya anwani mwafaka. (al.1)
2. Mwandishi anamaanisha nini anaposema kuwa dawa za kulevya ni donda ndugu katika taifa letu. (al.2)
3. Taja namna ambavyo dawa za kulevya zinavyotumiwa. (al.4)
4. Eleza athari ya dawa za kulevya kwa familia za wanaotumia . (al.2)
5. Kuna changamoto gani katika kupiga vita matumizi ya mihadararati. (al.1)
6. Eleza sera ya serikali kuhusu dawa za kulevya. (al.2)
More Examination Papers