TUTORKE EXAMS
102/3
KISWAHILI
FASIHI YA KISWAHILI
KIDATO CHA TATU
MUDA: SAA 21/2
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA TATU 2022
MAAGIZO:
• Jibu maswali MATATU pekee
• Swali la KWANZA ni la LAZIMA
• Maswali mengine yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki
• Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja
• Kila swali lina alama ishirini
SWALI LA KWANZA NI LA LAZIMA
1. SEHEMU YA D: USHAIRI
Ingawa mdogo, dagaa, amekomaa
Kaanga kidogo, dagaa, atakufaa
Kalia kinaya, dagaa, h’ondoa njaa
Wa kwako udogo, kijana, sio balaa
Na sio mzigo, kijana, bado wafaa
Toka kwa mtego, kijana, si nyanyapaa
Nasaha kidogo, kijana, ukubwa jaa
Jikaze kimbogo, kijana, achakukaa
Chimbua mhogo, kijana, usibung’aa
Na wake udogo, dagaa, ndani hukaa,
Kuliko vigogo, dagaa, hajambaa
Hapati kipigo, dagaa, hauna fazaa
Maisha si mwigo, kijana ushike taa
Si hofu magego, kijana, nawe wafaa
Kazana kidogo, kijana, kugaaga
Maswali
(a) Lipe shairi hili anwani mwafaka (alama 1)
(b) Eleza arudhi zilizofuatwa katika kutunga shairi hili (alama 4)
(c) Onyesha jinsi malenga alivyotumia uhuru wake (alama 3)
(d) Tambua bahari katika shairi hili (alama 3)
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari (alama 4)
(f) Tambua mbinu za lugha zilizotumika katika shairi (alama 3)
(g) Eleza toni la shairi hili (alama 2)
FASIHI SIMULIZI
2 i) Eleza umuhimu wa ngano za mtanziko katika jamii. (al.5)
(ii) Fafanua umuhimu wa maigizo ya watoto. (al.5)
(iii) Sifa tano za rara (al.5)
(iv) Eleza dhima ya misimu kama kipera cha usemi (al.5)
3. [a] Maigizo ni nini? ( al.2)
[b] Fafanua sifa nne za maigizo. Al.4)
[c] Eleza vikwazo vya ukuwaji wa fasihi simulizi. Al.10)
[d] Eleza tofauti kati ya misemo na misimu. Al.4)
TAMTHILIA YA KIGOGO (PAULINE KEA)
4.`…………….wanadai kitu kikumbwa au kitu chote!`
a) Eleza muktadha wa dondoo hili al 4
b) Tambua maudhui yanayodokezwa kwenye dondoo hili al 2
c) Kwa kutumia hoja sita eleza namna maudhui uliotaja hapo juu yanavyojitokeza katika tamthilia ya
kigogo. al 6
d) Fafanua sifa za msemewa al 4
e) fafanua umuhimu wa msemaji al 4
5: Jadili jinsi dhuluma inavyojitokeza katikaTamthilia ya Kigogo. (al 20)
CHOZI LA HERI- A. MATEI
6.“Mbona huna bashasha za kijana wa umri wako.”
a) Eleza muktadha wa maneno haya. la 4)
b) Ni yapi yalifuata baada ya maneno haya. ala 12)
c) Eleza sifa nne za msemewa ala 4)
7.“Riwaya ya Chozi la Heri inaakisi uozo uliomo katika Jamii nyingi barani Afrika”
Thibitisha kauli hii kwa kurejelea Riwaya al20